Kutokana na kutotii, Naibu Spika
aliamuru askari wamtoe ndipo walipoingia zaidi ya askari watano na kutoka naye
hadi nje ya geti kubwa la kuingilia bungeni.
Mhe.Holle wakati anachangia bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa
fedha 2016/2017, alimtaja Lissu ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara hiyo kuwa ana
taarifa kuwa Lissu amewahi kuugua ugonjwa wa kichaa na hadi sasa ana faili
kwenye Hospitali ya Vichaa ya Mirembe iliyopo mkoani Dodoma.
Hata hivyo, alipopewa nafasi na Naibu
Spika kufuta kauli yake akasema“nafuta kauli yangu lakini kwa taarifa zilizozagaa nimeamini
ni kweli na mbona kwao(Chadema) wapo wengi hata Mnyika sasa hivi yupo Muhimbili
anatibiwa kichaa”.
Kutokana na kauli hiyo, Lissu alisema
licha ya kuifahamu Hospitali ya Mirembe, hajawahi hata kuingia kwenye geti la
hospitali hiyo wala kuugua ugonjwa huo na kutaka kiti cha Naibu Spika kimtake
Holle athibitishe ; na akishindwa kanuni zielekeze hatua za kuchukua kama
zilivyowekwa.KWA PICHA ZAIDI ...BOFYA HAPA.
|
Friday, May 06, 2016
Home
SIASA
KUTOKA BUNGENI DODOMA:- Mhe.Mwita Waitara Azusha Tafrani Baada ya Kutaka Kumchapa Ngumi Mbunge wa Kasulu Aliyedai Tundu Lissu na Mnyika Ni Vichaa.
KUTOKA BUNGENI DODOMA:- Mhe.Mwita Waitara Azusha Tafrani Baada ya Kutaka Kumchapa Ngumi Mbunge wa Kasulu Aliyedai Tundu Lissu na Mnyika Ni Vichaa.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment