HABARI / VIDEO:-Binti wa Miaka 16 toka Mwanza,Tanzania awakilisha Vijana Ulimwenguni na kuhutubia Umoja wa Mataifa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 24, 2016

HABARI / VIDEO:-Binti wa Miaka 16 toka Mwanza,Tanzania awakilisha Vijana Ulimwenguni na kuhutubia Umoja wa Mataifa.

Getrude Clement ,Binti mwenye umri wa miaka 16 kutoka Jijini Mwanza,Nchini Tanzania amehutubia mbele ya Viongozi mbalimbali wa Dunia kwenye hafla maalum ya Mkutano wa Makubaliano ya Paris , Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), New York, Marekani kama mwakilishi mtandao wa wanahabari watoto wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani, UNICEF.

Getrude alipata nafasi ya kuwakilisha Vijana kutoka Ulimwenguni kote alipohutubia Baraza hilo akiwa mwenye kujiamini na kutoonekana kuwa na hofu japo anaongea kwenye jukwaa ambalo linatazamwa na viongozi mbalimbali.

 Mataifa zaidi ya 150 yalitia saini makubaliano ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo Marekani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Bw. Ban Ki Moon ndio alimkaribisha Getrude kuongea kwa kusema ‘’…ni furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni Mwakilishi wa Vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha Sauti za Vijana‘

Iliripotiwa Maraisi 60 walihudhuria na Getrude alianza kwa kuwasalimia waalikwa kisha …’’alizungumzia mabadiliko ya tabia nchi, hatari yake na kwamba wamekua wakifikisha ujumbe kwa Wananchi juu ya mabadiliko hayo.

..........Bonyeza HAPA CHINI Umsikilize kwenye hii video ..

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad