WABUNGE
WATATU WAJUMBE WA KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI
KWA RUSHWA
--
Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 31/3/2016 imewafikisha
Mahakamani Wabunge watatu ambao ni wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za
Mitaa kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa ya Shilingi Milioni thelathini
(30,000,000/-) kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya
mwaka 2007 kifungu cha 15 (i)(a).
Wabunge hao
ni Mheshimiwa Suleiman Ahmed Saddiq Mbunge wa Mvomero;Mheshimiwa Victor
Mwambalaswa Mbunge wa Lupa na Mheshimiwa Kangi Lugola Mbunge wa Mwibara.
Wabunge hao
wamesomewa shitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu
Mfawidhi, Mh.Thomas Simba.
Akisoma
mashtaka hayo wakili wa TAKUKURU, Maghera Ndimbo akishirikiana na Emmanuel
Jacob alisema kuwa mnamo Machi 3, 2016 majira ya saa 2 - 4 usiku, katika Hotel
ya Golden Tulip iliyopo jijini Dar es Salaam washtakiwa wote watatu waliomba
rushwa ya shilingi Mil.30 kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo kwa
lengo la kumsaidia ili Taarifa ya Halmashauri hiyo ambayo ilikuwa kwa wakati
huo ijadiliwe tahere 16/3/2016 ipitishwe
bila marekebisho.
Uchunguzi wa
shauri hili bado unaendelea na washtakiwa wote watatu mahakama imewaachia kwa
dhamana ya kila mtuhumiwa kuwa na mdhamini mmoja na kulipa shilingi milioni 5.
Kesi imeahirishwa hadi
tarehe 14/4/ 2016 itakapotajwa tena.
TAKUKURU
inawajulisha wananchi wote kwamba hakuna mtu ambaye yupo juu ya Sheria. Rushwa haivumiliki!
IMETOLEWA NA
OFISI YA
AFISA UHUSIANO
TAASISI YA
KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, MAKAO MAKUU
31 MACHI,
2016.
|
No comments:
Post a Comment