UHALIFU/PICHA:-Watu 6 Watiwa Mbaroni Kufuatia Kutunguliwa helikopta Katika Ranchi ya Wanyapori ya Mwiba, Meatu. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Tuesday, February 02, 2016

demo-image

UHALIFU/PICHA:-Watu 6 Watiwa Mbaroni Kufuatia Kutunguliwa helikopta Katika Ranchi ya Wanyapori ya Mwiba, Meatu.

.com/simgad/
1
Watu sita wanaodaiwa kuwa majangili, wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuitungua helikopta ya doria na kusababisha kifo cha rubani wake katika pori la akiba la Maswa.

Kukamatwa kwa watu hao kumekuja siku moja baada ya Rais, John Magufuli, kutoa agizo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwakamatwa waliohusika na tukio hilo na kufikishwa katika mkono ya sheria.

Kauli hiyo ya Rais iliyotolewa  na  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa,  ilisema Rais Magufuli mbali na kusikitishwa na tukio hilo, pia aliuakikisha umma kuwa serikali itahakikisha inaendeleza mapambano dhidi ya ujangili kwa nguvu zote na kuwataka wananchi na wadau mbalimbali wa hifadhi ya wanyamapori kutokatishwa tama.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Gemini Mushy, jana February 01,2016 alithibitisha  kukamatwa kwa watu hao.

Alisema awali walikamata watu wawili, juzi watatu na jana mmoja wote wakiwa wakazi wa Simiyu na uchunguzi bado unaendelea. 

Ijumaa iliyopita, watu wasiojulikana, waliitungua helikopta hiyo  wakati ikifanya doria katika pori hilo baada ya kuwapo taarifa kwamba majangili walikuwa wameua tembo mmoja.

Katika tukio hilo, rubani wa helikopta hiyo raia wa Uingereza, Rodgers Gower (37) alikufa, huku mwenzake Nicky Bester wa Afrika Kusini akinusurika.


Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630 .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *