![]() |
Bi. Kazijya
Kila ambaye ni mmoja wa wanufaikaji wa fedha akitoa ushuhuda kuhusu mradi wake
wa chakula ulivyowezeshwa na TASAF ambapo hadi hivi sasa anatengeneza faida ya
Shilingi 7000 kwa siku na kabla ya kuwezeshwa alikuwa akikaa nyumbani na mama
yake bila kuingiza kipato chochote.
Katika
Mpango huo ambao utekelezwaji wake unasimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) unafanyika Tanzania Bara na Tanzania visiwani ukiwa na lengo la
kuzisaidia kaya masikini pesa za matumizi ili kukidhi mahitaji ya kupata
chakula pamoja na kuwawezesha kusaidia watoto wao kupata elimu jambo ambalo
linaonekana kuzaa matunda kwa maeneo mengi ikiwepo Tanzania visiwani.
Serikali ya
Tanzania imekuwa ikisaidia na washirika wa maendeleo ili kupunguza umaskini
uliokithiri kwa wananchi wake na mwaka 2013 iliweka mpango wa kusaidia kaya
masikini 275,000 kwa kipindi cha miaka mitano na tangu ianzishe mpango huo
ilifanikiwa kusaidia kaya 275,000 kwa mwaka 2013 pekee katika wilaya nane
nchini.
|
![]() |
Mtaalamu
Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi
Mohamed (kushoto) na Msimamizi wa mpango wa PSSN, Bw. Ramadhani Madari
wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu kwa wanufaikaji wa fedha hizo.
Na mpaka
kufikia sasa mpango huo umeshatoa malipo mara 12 na jumla ya kaya masikini
milioni 1.1 zimeshafaidika na mpango huo ikiwa ni kwa wilaya 161 na vijiji 9789
nchini.
Malengo ya
serikali ya Tanzania na mashirika ya kimataifa ni kuhakikisha kufikia mwaka
2030 kunakuwa hakuna masikini hivyo ni wajibu wa kila nchi kuhakikisha
inawasaidia wananchi wake ili wajijengee uwezo wa kujitegemea na kuondoka
katika janga la umasikini.
|
![]() |
Asilimia
kubwa ya wanufaikaji wa mpango huo ni wanawake, kama wanavyoonekana pichani.
|
![]() |
Mkurugenzi
wa Huduma za jamii kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Amadeus
Kamagenge akizungumza na wanufaikaji wa mpango wa TASAF (hawapo pichani).
|
![]() |
Mkurugenzi
wa Huduma za jamii kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Amadeus
Kamagenge (kushoto) akifurahi jambo na Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Jamii
kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed.
|
![]() |
Timu ya
TASAF na wadau wa maendeleo wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri katika
mkutano huo.
|
![]() |
Mtaalamu
Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi
Mohamed na Aine Mushi wa UN/NRA.
|
No comments:
Post a Comment