VPL 2015/2016:-Yanga yatunguliwa Mkwakwani ….Simba SC yafufua Matumaini ya Ubingwa …Hapa Matokeo ya Mechi Leo January 30, 2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 30, 2016

VPL 2015/2016:-Yanga yatunguliwa Mkwakwani ….Simba SC yafufua Matumaini ya Ubingwa …Hapa Matokeo ya Mechi Leo January 30, 2016.

Wachezaji wa Simba wakishangilia moja ya magoli yao yalifungwa kwenye mchezo wa leo dhidi ya African Sports

Wachezaji wa Simba SC wakishangilia moja ya magoli yao yalifungwa kwenye mchezo wa leo January 30, 2016 dhidi ya African Sports.

Klabu ya Simba SC imeendelea kuzikimbiza Yanga SC na Azam FC katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu huu 2015/2016 baada ya kufanikiwa kuichapa African Sports kwa bao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya ligi hiyo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa.

Hamisi Kiiza ameibuka shujaa wa mchezo huo akifanikiwa kuweka bao mbili kambani ndani ya kipindi cha kwanza huku bao la tatu ndani ya kipindi cha kwanza likifungwa na Hasan Kessy.

Beki wa African Sports (kushoto) akimdhibiti Ibrahim Ajib wakati wa mchezo wa Simba vs African Sports

Beki wa African Sports (kushoto) akimdhibiti Ibrahim Ajib wakati wa mchezo wa Simba vs African Sports.

Bao la ushindi la Simba SC, limekwamishwa wavuni na Haji Ugando na kukamilisha kalamu ya mabao kwa siku ya leo.

Matumaini ya Simba SC kuibuka kidedea kwa kutwaa ndoo ya ligi msimu huu yameibuka baada ya mtani wao Yanga SC kukwama jijini Tanga mbele ya Coastal Union kwa kipigo cha bao 2-0. 

Azam FC ambao leo,January 30,2016, wangecheza na Tanzania Prisons hawapo nchini hivyo mchezo huo umeahirishwa hadi hapo watakaporejea nchini.

Haji Ugando akijaribu kumtoka Ally Ahmed wa African Sports

Haji Ugando akijaribu kumtoka Ally Ahmed wa African Sports

Yanga SC bado wanaongoza ligi wakiwa na pointi 39, Azam FC wako nafasi ya pili kwa pointi 39 sawa na Yanga SC lakini wao wanafaida ya mchezo mmoja mkononi ambao walitakiwa wacheze leo.

Raia wa kigeni waliovalia jezi nyekundu pia walikuwa wakishuhudia pambano kati ya Simba dhidi ya African Sports

Raia wa kigeni waliovalia jezi nyekundu pia walikuwa wakishuhudia pambano kati ya Simba SC dhidi ya African Sports.

Matokeo hayo yanaiingiza Simba SC kwenye orodha ya timu ambazo zinawania ubingwa msimu huu kutokana na tofauti ya pointi 3,Simba SC sasa wamefikisha pointi 36 lakini bado kuna mechi nyingi ambazo zinaweza zikaamua nani ataibuka bingwa wa msimu huu.
Ibrahim Ajib akichuana na Juma Shemvuni

Ibrahim Ajib akichuana na Juma Shemvuni

Kocha Jackson Mayanja ambaye anashikilia nafasi ya kocha mkuu kwa muda tangu kutimuliwa kwa Dylan Kerr ameendelea kufurahia ushindi ndani ya klabu hiyo kwani ameshinda mechi zote ambazo ameingoza Simba SC.

Kessy 6

Mayanja ameingoza Simba SC kwenye mechi tatu za ligi (Simba vs Mtibwa Sugar, Simba vs JKT Ruvu na Simba vs African Sports) na kuvuna ponti 9 katika michezo hiyo lakini paia alikiongoza kikosi hicho kwenye ushindi wa magoli 3-0 kwenye kombe la FA dhidi ya Burkina Faso ya mkoani Morogoro.
Mashabiki wa Simba wakiishanglia timu yao

Mashabiki wa Simba wakiishanglia timu yao.Picha kwa hisani ya shaffihdauda.

MATOKEO NA RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA  BARA 2015/2016.


Januari 30, 2016.

Coastal Union 2-0 Yanga SC

Simba SC 4-0 African Sports

JKT Ruvu 0-0 Majimaji

Mwadui FC 1-0 Toto Africans

Kagera Sugar Vs Mbeya City

Kesho; Januari 31, 2016.

Mgambo JKT Vs Ndanda FC

Mtibwa Sugar Vs Stand United

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630 .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad