Kufuatia
tukio hilo, waziri wa maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe amefika
katika eneo la tukio na kusisitiza kwamba serikali kwa kushirikiana na vyombo
vyote vya dola na vyombo vya ulinzi na usalama inaanzisha mkakati mpya wa
kupambana na ujangili na uwindaji haramu wa maliasili ikiwemo Tembo ambao ni
rasilimali muhimu kwa taifa na kwa uhifadhi wa taifa la Tanzania.
Waziri
Maghembe ambae amefika kwenye eneo hilo ilipotunguliwa na kuikuta helkopita
hiyo iliyokuwa inarushwa na kepten Roger Gower raia wa Uingereza ambae
alifariki baada ya kujeruhiwa kwa risasi amesema tukio hilo limewakera wadau
wote wa uhifadhi na serikali kwa ujumla na kamwe haliwezi kuachwa lipite bila
hatua madhubuti kuchukuliwa huku akiwaonya baadhi ya watumishi wa serikali na
askari wa wanyamapori wanaoshirikiana na wahalifu kuwa sasa kiama chao
kimefika.
|
Nae kamanda
wa upelelezi wa mkoa wa Simiyu Jonathan Shana amesema tukio hilo lilitokea jana
jioni wakati helkopita hiyo ikiwa katika doria baada ya kusikika milio ya
risasi ya majangili katika pori hilo ambapo Tembo watatu waliuwawa na kwamba
watu watatu wanashikiliwa na polisi wakihojiwa kufuatia tukio hilo.
Hili ni
tukio la kwanza katika historia ya
uhifadhi nchini mwetu kwa Majangili kumpiga
risasi na kumuua Rubani na kisha
kuangusha helikopta .
Kepten Roger
alikuwa akienda kuongeza nguvu ya askari wa uhifadhi waliokuwa wakipambana na
majangili hatari wilayani Meatu, Simiyu katika ranchi ya wanyamapori ya Mwiba.PICHA KWA HISANI YA MPEKUZI.
|
No comments:
Post a Comment