Mkuu wa Mkoa
Mhe. Mongella mara baada ya kuwahoji alikubaliana na Baraza la Madiwani kuwa
watendaji hao wanatakiwa kuwajibishwa na kuliagiza Baraza hilo kukaa kikao na
kuamua hatua ya kuchukua kwa wahusika wote kwani mamlaka ya kuwawajibisha Wakuu
wa Idara wa halmashauri ipo kwa Madiwani wenyewe.
Aidha,
alimwagiza Katibu Tawala Mkoa kumwadikia barua Katibu Mkuu TAMISEMI ili aweze
kumchukulia hatua Mkurugenzi Mtendaji Bi Gradis Dyamvunye aliyekuwepo wakati
huo na kuomba aliyekuwa Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri hiyo Robert Massoro
kurudishwa kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za mfuko wa barabara pia
kuomba ufanyike ukaguzi maalum mara moaja.
Kikao cha
Baraza la Madiwani kilichofanyika tarehe 28.01.2016 kikiongozwa na Mwenyekiti
wake Mustapha Ngeze kiliamua kwa kauli moja kuwasimamisha kazi kupisha
uchunguzi wa upotevu wa milioni 851 watendaji wafuatao; Idara ya fedha ni Bw.
Jonathan Katunzi (Mweka Hazina), Selialisi Mutalemwa, Idara ya Ujenzi, Bw. Deus
Bizibu, Elimu Sekondari ni Bw. Lucas Mzungu, Mifugo ni Dk. Kisanga Makigo na
Bw.Mustapha Sabuni Afisa Mipango.
Mchanganuo
wa fedha zilizotumika bila kufuata utaratibu na kanuni za fedha ni Shilingi
milioni 200 za mfuko maalum wa barabara zilizokuwa zimeletwa kwa ajili ya
kujenga daraja la Kyamabale, Milioni 176 za mfuko wa barabara kwa ajili ya
kutengeneza na kukarabati barabara, Milioni 168 za mfuko wa Jimbo, na Milioni
307 za mfuko wa Afya (Busket Fund).
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii,
Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha
kwa WhatsApp +255789925630 .
|
No comments:
Post a Comment