Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ameagiza na kusisitiza ofisi zote Umma kusimamia
na kuhakikisha kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu kila watumishi
awe na kitambulisho (BEJI) kinachoonesha jina lake.
Akiongea na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam Balozi Sefue alisema hatua hiyo ya
watumishi wa umma kuvaa beji zenye majina kila wakati wanapotekeleza majukumu
yao itasaidia wananchi kuwatambua kwa majina watumishi wanaowahudumia na
kuwasaidia kulingana na mahitaji yao kwenye ofisi hizo.
Ili
kutekeleza azma ya kuwahudumia wananchi, Balozi Sefue alisema kuwa kuanzia sasa
watumishi wote wa umma wavae beji zenye majina yao iwe rahisi kwa mwananchi
kumtambua anayemhudumia na hivyo kumsifu mtumishi wa umma anayewahudumia kwa
weledi, uaminifu na kwa wakati na kumtolea taarifa yule anayefanya mambo ya
hovyo.
Zaidi ya
hayo, Balozi Sefue amewahimiza viongozi na watumishi wote katika Utumishi wa
Umma kubadilika kwa dhati kwenye utendaji na uadilifu wao na kuwahudumia
wananchi kwa haki, weledi, uadilifu na heshima.
“Rais na
sisi wote tunaomsaidia hatuoni raha kuchukua hatua dhidi ya viongozi na
watumishi wengine, tungependa kila mtu mwenyewe ajirekebishe na kutomfikisha
Rais mahali ambapo inabidi amchukulie hatua” alisema Sefue.
Mambo muhimu
yanayopaswa kuzingatiwa ni pamoja na kila kiongozi na mamlaka ya nidhamu
isipate kigugumizi kusimamia utendaji na maadili ya kazi ili kuchukua hatua za
nidhamu, lakini afanye hivyo kwa kuzingatia kwa ukamilifu sheria, kanuni na
taratibu katika Utumishi wa Umma.
Balozi Sefue
amewahimza viongozi na watumishi wa umma kuwahudumia wananchi kwa haki, weledi,
uadilifu na heshima ambapo kila ofisi ya Serikali inapaswa kuwa na dawati la
kusikiliza shida za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Kwa upande
wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wote nchini wametakiwa
kujenga uwezo wa kushughulikia shida za wananchi kwa ukamilifu na kwa wakati.
“Kwa muundo
wa Serikali yetu hakuna sababu kwa mwananchi kufunga safari mpaka Ikulu Dar es
Salaam kwa kuamini kuwa ni Rais tu ndiye anayeweza kumaliza matatizo yake,
maana wawakilishi wa Rais wako kila pembe ya nchi yetu, ikibidi wananchi wafike
Ikulu inamaana hao wawakilishi wa Rais hawakutimiza wajibu wao” aliongeza
Balozi Sefue.
Aidha,
Balozi Sefue alisema kuwa ofisi zote za Serikali zinatakiwa kuwa na dawati la
kupokea maoni ya wananchi kuhusu huduma inayotolewa kwenye ofisi hizo na
kushughulikia haraka maeneo yote ambayo wananchi wataonesha kutoridhika na
huduma inayotolewa.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii,
Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha
kwa WhatsApp +255789925630 .
|
No comments:
Post a Comment