Kikao cha
pili cha Bunge la Kumi na Moja linalotarajiwa kuwa na ushindani mkali wa hoja
kati ya wabunge wa vya upinzani vinavyounda UKAWA na wabunge wa CCM kimeanza
leo,January 26,2016 mjini Dodoma huku mambo 8 muhimu yakitarajiwa kuibua mjadala mkubwa.
Jambo la
kwanza ni kujadili hotuba ya Rais John Magufuli aliyoitoa bungeni hapo mwaka
jana 2015 katika kikao cha kwanza cha bunge hilo. Hapo suala la kupambana na ufisadi
linatarajia kuleta hoja nzito zaidi kutoka kila upande. Hotuba ya Rais
ilisifiwa na takribani kila mwananchi pamoja na wanasiasa mbalimbali.
Jambo la Pili,
Kurudiwa kwa uchaguzi Mkuu wa Zanzibar. Hili ni suala nyeti na linalopaswa
kubebwa kwa uangalifu mkubwa.
Wabunge wa
UKAWA na CCM wanatarajiwa kurusha makombora yao ya hoja na maoni katika
kusaidia namna ya kupata muafaka. Bila shaka hapo mengi yataibuka na huenda
kukawa na mgongano mkubwa wa hoja na mawazo.
Jambo la Tatu, Zoezi
la Bomoabomoa pia linaweza kupewa nafasi yake katika Bunge hilo hususan katika
utekelezaji wake na mapungufu yaliyojitokeza.
Jambo la Nne,Maazimio
ya Bunge juu ya sakata la ESCROW linaweza kuwa mada moto zaidi katika bunge
hilo kwani tayari kumekuwa na vutankuvute kabla ya Bunge.
Mbunge wa
jimbo la Ubungo Saed Kubenea na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ambao ni
mahasimu wa kisiasa wameonekana kuwa na nia moja katika kulirudisha bungeni
sakata la ESCROW. Mmiliki wa Kampuni ya IPTL/PAP, Harbinder Singh Sethi
amepinga mahakamani kurudishwa bungeni kwa sakata hilo lakini Zitto amesisitiza
kuwa mtu binafsi hawezi kulizuia Bunge kutekeleza majukumu yake.
Jambo la Tano,Utekelezaji
wa sera ya elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne pia ni suala
ambalo litaleta mjadala katika Bunge hilo, kwa kuzingatia changamoto zilizoanza
kuripotiwa.
Jambo la Sita,Uteuzi
wa wajumbe wa kamati za Bunge ambao vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa
vimeulalamikia na hata kutishia kuususia unatarajiwa kuwa sehemu ya hoja
zitakazoleta mjadala mkubwa katika Bunge hilo.
Jambo la Saba,Ni migogoro
iliyoibuka katika chaguzi za Mameya wa majini na Manispaa pamoja na wenyeviti
wa Halmashauri. Waziri wa TAMISEMI atakuwa na kazi ya kujibu hoja na maswali
yatakayokuwa yanaelekezwa kwake kuhusu zoezi hilo.
Jambo la Nane, Hoja
binafsi za wabunge zinatarajiwa kuibuliwa na kuleta mjadala mzito kwani tayari
baadhi ya wabunge wamekwisha eleza nia yao ya kupeleka bungeni hoja binafsi
kuhusu masuala mbalimbali.
Bunge hili
linatarajiwa kuwa la kipekee na lenye
changamoto kubwa kwa kuwa na idadi kubwa ya vijana na idadi kubwa ya wabunge wa
upinzani ambao wameunda umoja wao.
|
Tuesday, January 26, 2016
Home
SIASA
WAWAKILISHI WETU:- Bunge la 11 Linaanza Leo January 26, 2016 na Haya ni mambo Nane yatakayowasha Moto Bungeni.
WAWAKILISHI WETU:- Bunge la 11 Linaanza Leo January 26, 2016 na Haya ni mambo Nane yatakayowasha Moto Bungeni.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment