Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Rebeca
Gyumi akizungumza jambo na Wakili wakujitegemea, Jebra Kambole baada ya kutoka
Mahakama Kuu ambako wamefungua hauri la Kikatiba la kupinga sheria ya ndoa
kifungu cha 13 na 17 vinavyoruhusu mtoto wa kike chini ya miaka 18 kufunga
ndoa.
Na Avila
Kakingo wa Globu ya Jamii.
VIFUNGU vya
sheria ya ndoa vinavyoruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka 18 vyapingwa
mahakama kuu leo jijini Dar es Salaam.
Vipengele
vinavyopingwa ni kifungu cha sheria cha 13 na 17 vya sheria ya ndoa (CAP 29 R.E
2002), sheria inayotoa mwanya kwa mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa
kibali cha mahakana na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi ambayo ni kinyume na ibara
ya 13, 12 na 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 19977 zinazotoa
haki ya usawa mbele ya sheria kutokubaguliwa, kuheshimu utu wa mtu na uhuru wa
kujieleza.
Kesi ya
kupinga vifungu vya sheria ya ndoa
vinavyoruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka 18 ni keshi ya kikatiba yenye namba tano ya
mwaka 2016 iliyofunguliwa na Mwanaharakati wa haki za binadamu, Rebeca Gyumi na
kusimamiwa na wakili Jebra Kambole wa Law Guards Advocate.
Akizungumza
na waandishi wa jijini Dar es Salaam leo Mwanaharakati wa Haki za Binadamu,
Rebeca Gyumi ameomba mahakama kuu
kufutia mbali vifungu vya sheria hivyo na kupandisha umri wa chini wa kuoa kwa wanaume na kuolewa kwa wanawake kuwa ni miaka
18.
Aidha Rebeca
amesema kuwa ndoa za utotoni kwa
wasichana ni ukiukwaji wa haki za binadamu pia kuzaa kwa msichana akiwa na umri
mdogo ni chanzo kikubwa cha matatizo ya Fistula na vifo vingi vya wajawazito.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii,
Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha
kwa WhatsApp +255789925630 .
|
No comments:
Post a Comment