Meneja wa
Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma Eng. Leornad Chimagu
(kulia),akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa kuhusu athari za mafuriko katika kingo za barabara ya
Gairo-Dodoma eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma.
|
Gari
likipita sehemu iliyoathirika zaidi katika eneo la Kibaigwa barabara kuu ya
Gairo-Dodoma.
|
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania, Profesa Makame Mbarawa amemwagiza Meneja wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu
kuhakikisha ukarabati wa barabara katika eneo la Kibaigwa unaanza Jumapili hii.
Profesa
Mbarawa ameyasema hayo alipokuwa akikagua athari za uharibifu wa barabara
zilizosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Iringa –
Dodoma na kusababisha mafuriko yanayoharibu kingo za barabara.
“Hakikisheni
Jumapili kazi ya ujenzi hapa inaanza na ikamilike kwa muda mfupi ili kutoathiri
huduma ya usafiri katika barabara hiyo kutokana na umuhimu wake”, alisema Prof.
Mbarawa.
Waziri
Mbarawa amewataka TANROADS washirikiane na Kikosi cha Usalama Barabarani
kudhibiti magari yanayoegeshwa katika maeneo yasiyo rasmi na hivyo kusababisha
ajali na uharibifu wa barabara hususani katika maeneo ya Dumila mkoani Morogoro
na Kibaigwa mkoani Dodoma.
Mapema
Waziri Mbarawa alikagua ujenzi wa kingo za barabara unaoendelea katika eneo la
Dumila mkoani Morogoro ambapo amemuagiza Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro
Eng. Dorothy Ntenga kuhakikisha ujenzi huo wa kudhibiti barabara na daraja la
Dumila unakamilika kabla ya Februari 15,2016 ili kukabiliana na mafuriko wakati wa
mvua za masika zinazokaribia kuanza.
“Chimbeni
mchanga kwenye mto ili kuwezesha maji kupita kwa urahisi na kuondoa tishio la
mafuriko yanayo athiri daraja hilo wakati wa mvua za masika”, alisisitiza
Waziri Mbarawa.
Naye Meneja
wa TANROADS Mkoa wa Morogoro, Eng. Dorothy Ntenga amesema ili kudhibiti
mafuriko katika eneo la Dumila juhudi zinaendelea kupunguza mchanga na hivyo
kuwezesha kupita maji kwa urahisi.
Profesa
Mbarawa alikuwa katika ziara ya kukagua athari za mafuriko katika barabara ya
Morogoro-Dodoma ambapo maeneo ya Dumila na Kibaigwa yameathirika zaidi.
Imetolewa
na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Tanzania.
|
No comments:
Post a Comment