Naibu Katibu
Mkuu CHADEMA Zanzibar Salum Mwalimu
akionesha nyaraka ambazo zinadaiwa
kufanyiwa ‘fojali’ zilizoelezea kuwa zinatoka tume. Hata hivyo UKAWA
wameeleza kuwa nyaraka hizo wanataraajia kuziwasilisha Jeshi la Polisi kwani
kuna baadhi ya vitu vimefojiwa huku vikibainisha kuwa vinatoka Tume hiyo ya
Taifa ya Uchaguzi.
|
Mstahiki
Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob akisalimiana na Mstahiki Meya wa Ilala,
Charles Koyeko. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
HALMASHAURI
ya jiji la Dar es Salaam imeahirisha uchaguzi wa meya wa Jiji uliokuwa ufanyike
leo,January 23, 2016 mpaka hapo tarehe itakapotangazwa baadaye.
Mkuu wa
Kitengo cha Itifaki na Uhusiano na Umma wa Jiji, Gaston Makwembe alisema
uchaguzi huo uliokuwa ufanyike leo saa nne asubuhi katika ukumbi wa Mmikutano
wa Karimjee, umeahirishwa.
Alisema
tarehe ya uchaguzi huo itapangwa baadaye na taarifa zitatolewa kwa wananchi
kupitia vyombo vya habari bila kueleza sababu ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
Uchaguzi huo
unatarajiwa kuwa na mvutano wa aina yake kati ya vyama vinavyounda na Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA) pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Diwani wa
Kata ya Vijibweni, Isaya Mwita (CHADEMA) ndiye atapeperusha bendera ya UKAWA
huku mgombea wa nafasi ya Naibu Meya akitarajiwa kutoka CUF.
Chama Cha
Mapinduzi (CCM ) wakiwakilishwa na Diwani wa Kinondoni, Yusuph Omary Yenga.
Inaelezwa
kuwa UKAWA wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kiti hicho kutokana na kuwa na
idadi kubwa ya madiwani ambapo wanaizidi CCM kwa jumla ya madiwani 13.
Ikiwa UKAWA
watafanikiwa kutwaa jiji hilo, itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya
Tanzania kwa wapinzani kuliongoza tangu kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi
nchini mwaka 1992.
Awali, Ofisa
Habari wa Chadema, Tumaini Makene, alitoa mwito kwa Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusimamia uchaguzi huo kwa amani na haki
ili usifanyike kama wa kumtafuta meya wa Ilala na Kinondoni uliokuwa na
mizengwe mingi.
|
No comments:
Post a Comment