TASWIRA PICHA:-Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kufungwa Kwa Muda Barabara Ya Mpanda – Koga – Tabora. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, January 28, 2016

TASWIRA PICHA:-Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kufungwa Kwa Muda Barabara Ya Mpanda – Koga – Tabora.

Mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya magharibi mwa nchi zimesababisha uharibifu mkubwa wa barabara inayounganisha miji ya Mpanda-Inyonga (Katavi ) na Sikonge (Tabora) baada ya maji katika daraja la mto Koga kushindwa kufuata mkondo wake.

Pichani ni gari likijaribu kuyapita maji yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini zimeleta madhara baada ya daraja la mto Koga, lililopo mpakani mwa mikoa ya Katavi na Tabora kufurika maji. Hali hiyo imesababisha foleni ndefu ya magari katika eneo la mto huo.
Tunapenda kutoa taarifa kwa Umma kuwa, Barabara ya Mpanda – Koga – Tabora imefungwa kwa muda kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini zilizosababisha kufurika kwa mto Koga na kufanya daraja la Koga, lililopo mpakani mwa Mikoa ya Katavi na Tabora kutopitika na hivyo kukata mawasiliano ya barabara katika mikoa hiyo

Kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya barabara kupitia daraja hilo, tunaomba wananchi kusitisha safari kwa kutumia barabara hiyo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza hadi hapo barabara hiyo itakapofunguliwa mara tu baada ya maji kupungua katika eneo hilo.

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imechukua hatua hiyo kwa mujibu wa Kifungu cha 41 (1) cha Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka 2007 na Kanuni ya 8 (1) ya Kanuni za Usimamizi za Barabara za Mwaka 2009.

Wizara, inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi hiki chote.

Imetolewa na:
Eng. Joseph Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI)
28/01/2016.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630 .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad