KUTOKA DODOMA LEO JANUARY 28,2016:- Wabunge wa Upinzani Watoka Bungeni tena Baada ya Kunyimwa Muongozo ili Waongee. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, January 28, 2016

KUTOKA DODOMA LEO JANUARY 28,2016:- Wabunge wa Upinzani Watoka Bungeni tena Baada ya Kunyimwa Muongozo ili Waongee.

Baadhi ya Wabunge wametoka nje ya Bunge la Tanzania leo January 28,2016,asubuhi baada ya Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kuzuia Wabunge wasiendelee na kuomba mwongozo.


Baada ya  kipindi cha Maswali na Majibu, yalifuata matangazo  na   baada ya Matangazo, wabunge wakaanza kuchangia hotuba ya Rais Magufuli .
Wakati hayo yakiendelea, wabunge kadhaa wa UKAWA akiwemo mbunge wa Ubungo(CHADEMA), Saed Kubenea walikuwa wakiomba muongo wa Naibu Spika ili waongee lakini hawakupewa nafasi.

Hali hiyo iliwakera wabunge wa upinzani  kwa madai kuwa wamezibwa midomo na hivyo wakaamua kutoka nje ya ukumbi wa bunge

>>>:-Wabunge wa CCM wanaendelea  kujadili Hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge hilo..''.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630 .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad