Wakati Bunge
likieleza kuwa haliwezi kuzuia vituo vya televisheni nchini kuonyesha moja kwa
moja matangazo ya shughuli za vikao vya Bunge, Serikali ya Tanzania imetoa sababu tatu za
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kupunguza matangazo hayo ya shughuli za
chombo hicho chenye mamlaka ya kutunga sheria.
Uamuzi wa
Serikali kuhusu TBC ulizua sintofahamu bungeni na kusababisha polisi kutumika
kuwatoa katika Ukumbi wa Bunge, wabunge wa upinzani waliokuwa wakishinikiza
kusitishwa kwa mjadala wa hotuba ya Rais John Magufuli, badala yake lijadiliwe
suala hilo la shirika hilo.
Naibu Katibu
wa Bunge, John Joel alisema jana January 28,2016,kuwa hakuna televisheni yenye mkataba na Bunge
kurusha moja kwa moja matangazo hayo, zote zinazorusha zinatumia gharama zao
wenyewe.
Baada ya TBC
kupunguza matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge, televisheni
zilizobaki ambazo zinarusha moja kwa moja matangazo hayo, ni Star TV kupitia
chaneli yake ya Star Bunge pamoja na Azam TV.
“Sisi hatuna mkataba nao, wao wanarusha kwa
gharama zao na Bunge haliwezi kuwazuia, labda waulizwe wenyewe kama wataendelea
kurusha matangazo hayo ama laa,” alisema Joel huku akisisitiza kuwa hakuna zuio
lolote.
Juzi,January 27,2016, jioni
Waziri wa Habari, Nape Nnauye alizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma
na kueleza sababu tatu za kupunguzwa kwa matangazo hayo.
Nape
aliitaja sababu ya kwanza kuwa ni kupunguza gharama za uendeshaji, “Kwa mwaka
TBC ilikuwa inatumia Sh4.2 bilioni kurusha moja kwa moja matangazo haya. Fedha
hizi hazilipwi na Bunge wala Serikali, zinatokana na matangazo madogo ya TBC,
sasa pia hesabu tangu 2005 mpaka sasa zimetumika kiasi gasi.”
Alisema
sababu nyingine ya kupunguza kurushwa kwa Bunge ni kutaka wafanyakazi wa
Serikali kufanya kazi kikamilifu, kwa madai kuwa wengi badala ya kufanya kazi
walikuwa wakifuatilia vipindi hivyo.
Alisema
utafiti uliofanywa na Serikali umebaini kuwa waendesha bodaboda, mamalishe,
wamachinga, wakulima, wafugaji na watu wenye shughuli nyingi wanashindwa
kufuatilia vipindi vya Bunge asubuhi na mchana kutokana na kubanwa na shughuli
zao.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii,
Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha
kwa WhatsApp +255789925630 .
|
No comments:
Post a Comment