|
Kwa upande
wake, ambaye ni Mathias Mathew ni afisa wa kampuni ya huduma za meli katika
mkoa wa Kagera, amethibitisha kutokea kwa hitilafu katika injini ya meli hiyo
na pia amesema kuwa meli itaendelea na safari zake, huku, Patric Machia, afisa
mfawidhi wa mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA) na mkaguzi wa
mamlaka hiyo wa vyombo vya majini katika mkoa wa Kagera, akieleza kuwa meli hiyo
haitaruhusiwa kuondoka katika bandari ya Bukoba kwa kutumia injini moja.
Meli ya Mv.
Serengeti mara kwa mara imekuwa ikipoteza mwelekeo pale inapokumbana na dhuruba
na wakati mwingine injini za meli hiyo zimekuwa zikizimika mara kwa mara hali
ambayo pia inahatarisha usalama wa abiria na mali zao, meli ya Mv serengeti ni
mbadala ya meli ya Mv Victoria iliyoko kwenye matengenezo kwa sasa ambavyo hadi
sasa yameishachukua kipindi cha zaidi ya miaka mitatu.
|
No comments:
Post a Comment