MAPINDUZI CUP 2016:-Ratiba ya Nusu Fainali January 10..Simba na Mtibwa...Yanga na URA. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 09, 2016

MAPINDUZI CUP 2016:-Ratiba ya Nusu Fainali January 10..Simba na Mtibwa...Yanga na URA.

Mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi,Klabu ya Simba SC sasa itacheza na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa nusu fainali wa michuano ya Mapinduzi Cup 2016 baada kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya JKU ya Zanzibar mchezo uliochezwa January 9, 2016 usiku kwenye uwanja wa Amaan.
Kiungo wa ‘Wekundu wa Maimbazi’ Simba SC, Jonas Mkude ndiye aliyeinusuru timu yake ambayo ilikuwa inahaha kutafuta bao kwa kila mbinu, dakika ya 65 Mkude akaifungia Simba SC bao pekee lililoipa tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali ikiwa kinara wa kundi A.
Kutokana na Simba SC kuongoza kundi, itachuana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa nusu fainali. 

Mtibwa itacheza na Simba kwenye mchezo huo kufuatia kumaliza ikiwa nafasi ya pili kwenye kundi lake nyuma ya Yanga SC.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga SC watakutana na URA ya Uganda ambayo imemaliza ikiwa katika nafasi ya pili katika kundi lake wakati Yanga SC wao wamemaliza wakiwa vinara wa kundi B.

Ratiba  ya nusu fainali ya Mapinduzi Cup 2016.

Jumapili January 10, 2016.

Saa 10:15 jioni: Mtibwa Sugar vs Simba SC

Saa 2:15 usiku: Yanga SC vs URA FC

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad