KIVUKO MTO KILOMBERO KUZAMA:- Watu 30 wameokolewa kati ya 31, uokozi unaendelea…Picha zaidi hapa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, January 28, 2016

KIVUKO MTO KILOMBERO KUZAMA:- Watu 30 wameokolewa kati ya 31, uokozi unaendelea…Picha zaidi hapa.

Watu wapatao 30 wameokolewa mpaka sasa baada ya kivuko cha Mto Kilombero kushindwa kuhimili upepo na mawimbi mkali ulioambatana na mvua yaliyopelekea kivuko hicho kugonga nguzo za pembeni ya mto na kukosa mwelekeo hivyo kupinduka ndani ya maji,katika  ajali hiyo iliyotokea jana January 27,2016 Majira ya saa 1 usiku wakati kivuko hicho kikitokea Ulanga.

Tukio la kivuko hicho cha Mto Kilombero kushindwa kumudu hali ya hewa ,sio mara ya kwanza kujitokeza katika eneo hilo la mpakani mwa Wilaya za Kilombero na Ulanga, ambapo juzi hali kama hiyo ilijitokeza pia.



Muonekano wa Misingi ya Daraja la Mto huo, huku kivuko kilichozama kikionekana kulia.
Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama,Bi. Jenista Mhagama akatoa ufafanuzi ndani ya Bunge leo January 28,2016, kwamba ni kweli ajali hiyo imetokea, kivuko kimezama kikiwa kimepakia watu na magari.

Waziri Mhagama amesema watu 30 wameokolewa kati ya watu 31, jitihada zinaendelea kuokoa watu pamoja na mali.


Picha kwa hisani ya:- Michuzi Blog



Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630 .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad