EMIRATES FA CUP:- MK Dons 1- 5 Chelsea …Sasa Usoni kwa Manchester City. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Sunday, January 31, 2016

demo-image

EMIRATES FA CUP:- MK Dons 1- 5 Chelsea …Sasa Usoni kwa Manchester City.

.com/simgad/
3
Hetitriki ya Oscar, Bao la Eden Hazard la Penati, ikiwa ni Bao lake la kwanza katika Mechi 28, na lile la Bertrand Traore, limewapa Chelsea ushindi wa 5-1 walipocheza na MK Dons katika Mechi ya Raundi ya 4 ya EMIRATES FA CUP iliyochezwa huko mk Denbigh Stadium, Mjini Milton Keynes.

Mapema Leo,January 31, 2016 Everton nao walitinga Raundi ya 5 kwa kushinda Ugenini kwa kuichapa Carlisle 3-0 kwa Bao za Arouna Kone, Aaaron Lennon na Ross Barkley.
1
Mshambuliaji Diego Costa akimkabidhi mpira Oscar dos Santos Emboaba Junior baada ya kufunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa 5-1 dhidi ya MK Dons Uwanja wa MK.
2

1
Pia baada ya mechi hizo, DROO ya Mechi za Raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP imefanyika na kuzua Bigi Mechi kati ya Chelsea na Manchester City wakati Mabingwa Watetezi wa Kombe hili Arsenal, wakiwa Nyumbani kucheza na Hull City.

Manchester United wako Ugenini kucheza na Timu ya Daraja la chini Shrewsbury Town.

Zipo Mechi za Timu za Ligi Kuu , pekee ambapo Tottenham wako kwao kucheza na Crystal Palace na Bournemouth kuivaa Everton.
2
DROO YA RAUNDI YA 5

**Mechi kuchezwa Wikiendi ya Februari 19 hadi 22,2016.

Chelsea v Manchester City

Reading v West Brom au Peterborough

Watford v Leeds United

Shrewsbury Town v Manchester United

Blackburn v Liverpool au West Ham

Tottenham v Crystal Palace

Arsenal v Hull

Bournemouth v Everton


THE EMIRATES FA CUP 2015/16

TAREHE MUHIMU

Raundi ya 3

Ijumaa 9 Januari 2016

Raundi ya 4

Jumamosi 30 Januari 2016

Raundi ya 5

Jumamosi 20 Februari 2016

Raundi ya 6-Robo Fainali

Jumamosi 12 Machi 2016

Nusu Fainali

Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016

Fainali

Jumamosi 21 Mei 2016


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630 .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *