AJALI / PICHA:-Watu wawili wamefariki Dunia na wengine Kujeruhiwa katika ajali ya basi la BM Morogoro. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 23, 2016

AJALI / PICHA:-Watu wawili wamefariki Dunia na wengine Kujeruhiwa katika ajali ya basi la BM Morogoro.

Watu wawili wamefariki Dunia na wengine 42 kujeruhiwa, kati yao wanne vibaya baàda ya basi walilokuwa wakisafiria kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Morogoro, mali ya kampuni ya BM kuligonga ubavuni lori lililokuwa likija mbele yake na kuangukia kwenye bonde pembeni ya barabara na kupinduka mara nne, katika eneo la Lubungo Mikese, barabara  kuu ya Morogoro-Dar es Salaam.

Katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro na  majeruhi wa basi hilo la kampuni ya BM, wamejeruhiwa zaidi maeneo ya kichwani, usoni na miguuni, ambapo wameendelea kupatiwa matibabu huku baadhi ya waliohojiwa wameeleza namna ajali hiyo ilivyotokea na kulalamikia wizi uliofanywa na waliofika eneo la tukio baada ya ajali.

Daktari bingwa wa upasuaji katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, Francis Semwene amekiti kupokea miili ya wanaume wawili na majeruhi 42, ambapo wanne kati yao hali zao ni mbaya na wengine italazimika kuwakata baadhi ya viungo iwapo watashindikana kushonwa.


Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo akizungumzia ajali hiyo, amesema chanzo ni mwendo kasi na imetokea majira ya saa 3:30 usiku ikihuhusisha basi la mwisho kutoka jijini Dar es Salaam kuja Morogoro, mali ya kampuni ya BM, baada ya dereva wake kufika Lubungo eneo lenye kona na mteremko mkali, na akiwa mwendo kasi, kukutana mbele na lori likiwa na tela, likitokea uelekeo wa Morogoro kuelekea Dar es Salaam, likiwa linamalizia kupita lori jingine lililokuwa limeegesha barabarani baàda ya kuharibika, ambapo dereva wa basi aligonga tela la lori hilo lililokuwa kwenye mwendo na kukosa uelekeo na kupindukia bondeni na kusababisha vifo na majeruhi hao.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630 .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad