UCHAGUZI JIMBONI:-Ni Lema tena Arusha Mjini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, December 14, 2015

UCHAGUZI JIMBONI:-Ni Lema tena Arusha Mjini.

Mbunge Mteule wa Arusha Mjini, Godbless Lema akiwa na Aliyekuwa Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa
Mbunge Mteule wa Arusha Mjini, Godbless Lema akiwa na Aliyekuwa Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa

MGOMBEA Ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Arusha Mjini, Godblees Lema ameibuka mshindi na kutangazwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo.

     Katika uchaguzi huo ulioshirikisha vyama vitano vya siasa, Lema amepata kura 68,848 kati ya kura 104,353 zilizopigwa sawa na asilimia 65.9 akifuatiwa na Mgombea wa CCM, Philemon Mollel aliyepata kura 35.907 sawa na asilimia 34.4.

Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo ni Navo Mollel wa ACT-Maendeleo aliyepata kura 342 sawa na asilimia 03, Zuberi Mwinyi wa CUF aliyepata kura 106, sawa na asilimia 0.1, na Makama Rashidi wa NRA aliyepata kura 43 sawa na asilimia 0.04.

Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Juma Iddy, jimbo la Arusha wapiga kura walioandikishwa ni 317.814, na waliojtokeza kupiga kura ni 105,800 sawa na asilimia 32.83 na kura halali ni 104,353.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad