SAD NEWS:- Basi la Takbir Lagongana na Lori Desember 01,2015 usiku na Kuua Watu 12 Papo Hapo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, December 02, 2015

SAD NEWS:- Basi la Takbir Lagongana na Lori Desember 01,2015 usiku na Kuua Watu 12 Papo Hapo.

Watu 12 wamekufa papo hapo na wengine 18 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Taqbiir kugongana na lori la mafuta mkoani Singida.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi,Thobias Sedoyeka ameithibitishia , kutokea kwa ajali hiyo na kusema basi lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Katoro mkoani Geita.

 Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 1:30 usiku jana ,Desember 01,2015 katika eneo Kizonzo Wilaya ya Iramba mkoani Singida ma ilihusisha basi aina ya Scania lenye namba za usajili T230 BRJ lililokuwa likiendeshwa na Charles Kikaena lililogongana na lori la mafuta T793 CBH lililokuwa na tela T273CBH lilokuwa likiendeshwa na dereva Mohamed Rajabu.

Chanzo cha ajali ni dereva wa basi aliyekua akilipita lori mali ya kampuni ya Coca Cola T314CTS lililokuwa na tela T196 BEF na kugongana na lori la mafuta na kisha lori hilo kulichana basi kuanzia mbele upande wa dereva hadi mwisho na kusababisha vifo hivyo vya watu 12 na majeruhi 18 na basi hilo lilikuwa na aburia 51.

Miongoni mwa waliokufa wanaume ni saba akiwemo mtoto mdogo mmoja na wanawake watano kati yao watoto wawili. 

Majeruhi wa ajali hiyo walifikishwa katika Hospitali ya serikali ya Kiomboi mkoani Singida kwa matibabu.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .


Post Bottom Ad