R.I.P..:- Kasongo Mpinda ‘Clayton’ afariki dunia. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, December 03, 2015

R.I.P..:- Kasongo Mpinda ‘Clayton’ afariki dunia.

king kiki na kasongo
King Kiki (kulia) akiimba sambamba na Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ enzi za uhai wake.

Na Sifael Paul

Habari zilizoufikia mtandao huu jioni hii zinaeleza kuwa mwanamuziki mkongwe katika tasnia ya muziki wa dansi nchini mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ amefariki dunia nyumbani kwake, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa wanamuziki waliofanya naye kazi kwa muda mrefu, Kasongo ambaye alifanya kazi na bendi nyingi kama Maquis du Ziare akiwika na Nyimbo za Angelo, Mwana Malole, Nasononeka, Baharia, Siri ya Mkoko na zingine kibao amefariki dunia baada ya kuumwa kwa muda mrefu akisumbuliwa na Kisukari hivyo taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia yake.

Katika siku za mwishoni, Kasongo aliitumikia Bendi ya Bakulutu kabla ya kujiunga katika Bendi ya Bana Maquis ikiwa chini ya Tshimanga Kalala Asssosa.
kasongo
Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ akiwa na Issa Nundu (kulia).

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

Post Bottom Ad