CAPITAL ONE CUP:- Matokeo ya mechi za Desember 01,2015 yakiwapa Everton,Stoke City na Man City hatua ya Nusu Fainali.! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, December 02, 2015

CAPITAL ONE CUP:- Matokeo ya mechi za Desember 01,2015 yakiwapa Everton,Stoke City na Man City hatua ya Nusu Fainali.!

Timu ya  Everton, Stoke na Manchester City zote toka Ligi kuu Uingereza,zimefanikiwa kuingia Nusu Fainali za Kombe la Ligi huko Uingereza, ambalo hujulikana kama Capital One Cup, baada ya kushinda Mechi zao za Robo Fainali jana Desember 01,2015 dhidi ya Timu za Madaraja ya chini.

Wakiwa kwao Etihad, Manchester City waliichapa Hull City Bao 4-1 baada ya kuongoza 4-0 kwa Bao za Wilfied Bony, Kelechi Iheanacho na Bao 2 za Kevin De Bruyne na Hull City kupata Bao lao moja Dakika za mwishoni kupitia Andrew Robertson.

 Everton, wakicheza Ugenini huko Riverside Stadium, waliifunga Middlesbrough Bao 2-0 kwa Bao za Kipindi cha Kwanza za Gerard Deulofeu na Romelu Lukaku.

Nako huko Britannia Stadium, Stoke City waliipiga Sheffield Wednesday Bao 2-0 kwa Bao zilizofungwa na Ibrahim Afellay na Phil Bardsley.

Hii ni mara ya kwanza kwa Stoke City kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Ligi tangu Mwaka 1972 walipotwaa Kombe hili.

Leo Jumatano Desember 02,2015, ipo Mechi ya mwisho ya Robo Fainali ya Kombe hili wakati Timu za Ligi Kuu pekee zitakapocheza na ni kati ya Southampton na Liverpool.

Capital One Cup

Robo Fainali

**Mechi kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku

Jumatano Desemba 2,2015.

Southampton v Liverpool

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad