BARAZA LA HALMASHAURI YA NGARA:- Lamchagua Bw Erick Nkilamachumu kuwa Mwenyekiti. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, December 10, 2015

BARAZA LA HALMASHAURI YA NGARA:- Lamchagua Bw Erick Nkilamachumu kuwa Mwenyekiti.


Pichani ni Mwenyekiti Mpya wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera ambaye pia ni Diwani Mteule wa Kata ya Bukirilo (CCM )  Bw Erick Nkilamachumu ameshinda nafasi hiyo ya Uenyekiti leo December 10,2015 kwa Kuchaguliwa na Madiwani wa Halmashauri hiyo  kwa kupata kura 30.

Awali Bw Nkilamachumu alichaguliwa na Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mdogo wa chama hicho ,kwa kupata Kura 20 na kumshinda Bw George Kagomba aliyepata Kura 11 kati ya 31 zilizopigwa.

 Bw Erick Nkilamachumu anarithi nafasi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Diwani wa Kata ya Kibinga CCM-Bw John Shimilimana ambaye hakujitokeza kugombea tena.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara,mkoani Kagera aliyechaguliwa kuwa kura 30 na pia   Diwani Mteule wa Kata ya Rusumo, Bw Wilbad Bambala ( CCM)  yeye alishinda kwenye uchaguzi wa chama kwa kupata kura 16 dhidi ya Kura 15 alizopata mshindani wake Bw Philbert Kiiza
 

Naye  Diwani Mteule wa Kata ya Murukulazo Bw Mukiza Byamungu ( CCM) amechaguliwa kuwa Katibu wa Kamati ya Madiwani wa Halmashauri hiyo kwa kupigiwa kura 27 za Ndiyo dhidi ya Kura 4 za Hapana.


 Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad