![]() |
|
Baadhi ya
waandishi wa habari wakimsikiliza aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Mungano wa Tanzania, Anne Makinda leo jijini Dar es Salaam.
|
![]() |
|
Aliyekuwa
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza nao
leo katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila Kakingo,
Globu ya Jamii)
Aliyekuwa
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda amejing'atua
rasmi na kuachana na uongozi katika siasa kutokana na kufanya kazi za Siasa kwa
miaka 40.
Ameyasema
hayo alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Bunge
jijini Dar es Salaam leo November 13,2015.
Anne amesema kuwa "Sitagombea nafasi ya Uspika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala sitachukua fomu ya kugombea
nafasi ya uspika wala sifikilii kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya
Uspika"
Aidha Anne
amesema kuwa katika awamu yake ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa
Tanzania kulikuwa na changamoto nyingi kutokana na kuwepo na wabunge vijana.
Hata hivyo
kuwa na changamoto nyingi ila amesema kuwa alilifurahiya sana Bunge hilo
kutokana na kuwaelewa wabunge mbalimbali tabia zao hasa wakiwa Bungeni.
Anne
amepsema kuwa Spika wa sasa atakaye shinda nafasi awe si mwepesi wa kukasirika
kutokana na changamoto atakazo zipata Bungeni wakati wakijadilia masuala
mbalimbali ya Serikali, pia awe mtulivu na kukabiliana na changamoto zitakazo
jitokeza.
|








No comments:
Post a Comment