TANZIA :- Miili ya Askari wa JKT Bulombora waliofariki katika ajali Mkoani Kigoma yaagwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, October 02, 2015

TANZIA :- Miili ya Askari wa JKT Bulombora waliofariki katika ajali Mkoani Kigoma yaagwa.

Katibu Tawala wa mkoa Kigoma Injinia John Ndunguru (kushoto) akiongoza kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kigoma kuaga miili ya vijana wa jeshi la kujenga Taifa waliofariki kwenye ajali ya gari jana October 01,2015 nje kidogo ya manispaa ya kigoma ujiji ,vijana hao wamesafirishwa kuelekea makwao kwa taratibu za mazishi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Eng. John Ndunguru, leo October 02,2015 ,mchana amewaongoza waombolezaji kuaga miili ya askari saba wa Jeshi la Kujenga Taifa Kikosi cha 821KJ Kambi ya Bulombora mkoani Kigoma, ambao wamefariki dunia jana katika ajali ya gari.

Akiongea kwa niaba ya serikali wakati wa kuaga miili ya askari hao ambao wawili kati yao walikuwa askari wa kudumu na watano wa kujitolea, John Ndunguru, ametoa pole kwa wafiwa wote sambamba na kuwataka wananchi pamoja na uongozi wa jeshi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha majonzi.

Eng.John Ndunguru alisema kuwa serekali ya mkoa imepokea kwa masikitiko makubwa vifo vya askari hao saba na watashirikiana na wafiwa bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu. 
 
"Serekali ya mkoa ina masikitiko makubwa kwa kupokea habari hizi za kuondokewa na askari wetu tutashikiriana na wafiwa katika kipindi hiki kigumu"alisema Ndunguru.

 Askari kutoka vikosi na majeshi mbalimbali wakiwa mbele ya majeneza ya askari wenzao wa kikosi cha 821 JKT Bulombora waliofariki  kwa ajali kwaajili ya kutoa heshima za mwisho.
Baadhi ya viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Kigoma wakitoa heshima zao za mwisho kwa askari  wa kikosi cha 821 JKT bulombora waliopata ajali ya gari jana na kufariki dunia.

Mkuu wa kambi ya JKT Bulombora kikosi cha 821 Luteni Kanali Mohamed Mketo (kushoto) akitoa heshima kwa vijana wa JKT waliofariki kwa ajali ya gari mkoani Kigoma juzi ambapo vijana hao walisafirishwa jana kuelekea kwenye mikoa yao kwa mazishi.
Baadhi ya wanajeshi wa jeshi la wananchi wa Tanzania na wapiganaji kutoka JKT Bulombora wakitoa heshima kuaga miili ya vijana wa JKT waliofariki kwa ajali ya gari juzi mjini Kigoma.



Ajali hiyo ilitokea jana October 01,2015, jioni majira ya saa kumi na nusu katika kijiji cha Kasaka eneo la mzani, wakati askari hao wakisafiri kutoka kikosini Bulombora kwenda mjini Kigoma kikazi kwa kutumia gari lenye namba 57117 JW 09 mali ya jeshi, ambalo lilipasuka tairi zote za nyuma na kupoteza uelekeo.

Akiongea na waombolezaji waliofika katika viwanja vya hospitali ya mkoa wa kigoma(Maweni)kwaajili ya kuaga miili ya marehemu Mkuu wa vikosi vya Kigoma, Kanali Msuya alisema jeshi limepoteza nguvu kazi ya Taifa .

Alisema mpaka sasa taratibu zote za kusafirisha miili hiyo zimeshakamilika miili yote itaondoka kwa usafiri wa magari hadi mwanza na kesho watasafirishwa na ndege ya jeshi kwenda dar es salaam kwaajili ya kupelekwa kwenye mikoa yao kwa maziko.

Kanali msuya aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni MT 54407 SGT Ally Kambangwa mkazi wa mtwara,MT 108151 PTE Abeli Maisha mkazi morogoro,SM Eugini Bitati mkazi wa kibondo.

Wengine ni AH 7190 SM Saidi Sadara mkazi wa Shinyanga,RES Bakari Kibaya mkazi wa Tanga,RES Fredrick Kahemela mkazi wa arusha.

Msuya aliwataja majeruhi pia majina yao kuwa ni Benadicto Ndokeye,Raphael Yohana,Athanas Emanuel,Abuu Nzoge,Abubakari peter,Abubakari Msubi na Denis Manyanya.

Wengine ni Edward Nyanda,Elias Magessa,Gofrey Maliki,King Kasefu,Kamilius Agida,Stive Denis,Saidi Omary,Saidi Zuberi,Shabaani Zakari,victor John,Jackson Nyarubu na Mohamed Nyimbo.

Askari wengine 22 ambao wamejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni, kufuatia ajali hiyo, wametajwa kuwa ni Benedicto Ndokeye, Raphael Kibamba, Antanas Emmanuel, Abuu Nzoghe Hassan, Abubakar Mathias Peter, Bakari Sinuki Mwaisunga, Deus Manyanya Charles, Peter Edward Nyanda, Elias Masaga Magesa, Geofrey Peter Malik na King Lucas Kasofu.

Wengine ni Camilius William Hagida, Lameck John, Martin Andrew Lupatu, Steven Denis Mtege, Said Omary Kitogo, Said Suleiman Zuberi, Shabani Idd Zakaria, Victor Adelbert, Jackson John Nyarubi, Mohamed Jackson Nyimbo na Abubakar Hassan Mkubi, ambao kulingana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dr.Fadhil Kibaya wengi hali zao zinaendelea vizuri.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.    

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad