TAFAKARI YETU:- Taswira Picha Wauguzi wasambaratishwa na Polisi kwa kupewa dakika 30 kuondoka eneo la Mkutano. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, October 02, 2015

TAFAKARI YETU:- Taswira Picha Wauguzi wasambaratishwa na Polisi kwa kupewa dakika 30 kuondoka eneo la Mkutano.

Kauli ya 'TUNATAKA MABADILIKO' iliyotolewa na Wauguzi kupitia tamko lao lilotolewa na Rais wao katika mkutano wao mkuu unaoendelea mjini bukoba mkoani Kagera imewatokea puani baada ya serikali kuwataka kusitisha mkutano wao huo na kutawanyika katika viwanja ya St thereza unakoendelea mkutano huo.

Awali mkutano huo ulipangwa kumalizika leo October 02,2015, majira ya jioni na kuambatana na sherehe kubwa ambapo sasa  Rais wao ametoa tangazo kuwa mkutano huo umevunjwa kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Aidha taarifa zilizothibtishwa ni kuwa hata sherehe kubwa ya kupongezana iliyokuwa ifanyike leo usiku baina ya wauguzi hao kama utaratibu wao wa kila mwaka imefutwa kutokana na sekeseke hilo.

Aidha watoa huduma waliokuwa katika viwanja vya mkutano huo kama waliofunga matenti,vifaa vya matangazo,umeme,wapiga picha na wauza picha,wauza nguo nk wameamuliwa kuondoka eneo hilo ndani ya dk 30.TAZAMA PICHA NA KUSOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA.

Hapa chini ni baadi ya picha ya kile kilichtokea



Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.    

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad