Mahakama Kuu Dar es Salaam leo October 23,201`5 imetupilia mbali shauri la tafsiri ya sheria ya mpigakura kukaa au kutokaa umbali wa mitaa 200 kutoka eneo la kupiga kura.
Kwa mujibu wa majaji waliotoa maamuzi hayo wamesema kuwa, kwa kuwa mikutano ilishakatazwa kuwepo siku ya uchaguzi, hivyo hakuna mkutano, mkusanyiko au vikundi vyovyote vitakavyoruhisiwa siku hiyo na kufanya hivyo ni kuvunja sheria.
Pia wameeleza kuwa siku ya uchaguzi mtu yeyote atakayevaa sare ya chama chochote naye atakuwa amevunja sheria.Kwa upande wa wakili wa utetezi, Peter Kibatala amesema ameyapokea maamuzi hayo lakini atakata rufaa juu ya shauri hilo kwa manufaa ya chaguzi nyingine zijazo.
(NA DENIS MTIMA/GPL)
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
No comments:
Post a Comment