TUZO 2014/2015:- FC Barcelona na Arsenal wabeba tuzo kutoka Chama cha Klabu za Soka Ulaya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 08, 2015

TUZO 2014/2015:- FC Barcelona na Arsenal wabeba tuzo kutoka Chama cha Klabu za Soka Ulaya.

FC Barcelona wamezoa Tuzo ya Klabu Bora Ulaya kwa Msimu wa 2014/15 iliyotolewa na Chama cha Klabu za Soka Ulaya, ECA- (European Club Association).

 Tuzo hiyo kwa Barcelona imekuja baada ya wao kutwaa Trebo, yaani Ubingwa wa La Liga, Copa del Rey na UEFA Champions League Msimu uliopita 2014/2015.

Sherehe za utoaji Tuzo zilifanyika Jana Sepetember 07,2015, huko Geneva, Uswisi na Tuzo nyingine walitwaa Klabu ya Ukraine FC Dnipro Dnipropetrovsk waliopewa Tuzo ya Maendeleo Bora Mchezoni kwa kufika Fainali ya EUROPA League 2014/2015 bila kutarajiwa na kufungwa na Sevilla ya Spain.

Tuzo ya Ubora kwa Jamii na Programu Bora za Kijamii ilikwenda kwa Arsenal ambao wametambuliwa kwa mchango wao mkubwa kwa Jamii ya Jiji la London kukabiliana na tatizo la ajira kwa Vijana.

Tuzo ya 4 iliyotolewa na ECA ni ile ya Mafanikio Bora ambayo ilibebwa na Klabu ya Estonia Levadia Tallinn kwa mpango wao uitwao  'Pamoja Tutasonga' ambao ulilenga kusaidia Walemavu wanaohitaji msaada wa kuongozwa na Mbwa ili kuingia kirahisi Uwanjani kwa ajili ya Mechi.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad