TAZAMA VIDEO :-Dk. Slaa alivyo tangaza rasmi kuachana na Siasa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 02, 2015

TAZAMA VIDEO :-Dk. Slaa alivyo tangaza rasmi kuachana na Siasa.

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Willibrod Slaa ametangaza rasmi kuachana na siasa.

 Amesema hatua hiyo inatokana na hatua ya CHADEMA kumkaribisha Edward Lowassa bila masharti na baadaye kumteua kuwa mgombea urais wa chama hicho.

Lowassa ambaye ni mgombea urais wa CHADEMA, anaungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambavyo ni CHADEMA yenyewe, CUF, NCCR-Mageuzi pamoja na NLD.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana September 01,2015 ,jijini Dar es Salaam, Dk. Slaa amesema hatojiunga na chama chochote cha siasa na badala yake ataendelea kuwatumikia wananchi nje ya siasa.

Hata hivyo amesema uamuzi huo unatokana na kutoridhishwa na hatua zilizochukuliwa na viongozi wakuu wa CHADEMA akiwemo mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kupokea wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliowahi kutuhumiwa na chama hicho.

BOFYA HAPA CHINI KUTAZAMA VIDEO YA MKUTANO WAKE NA WAANDISHI WA HABARI.

 

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad