![]() |
|
Mgombea
mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwa
amepokea kadi kutoka kwa wanachama wa CHADEMA waliojiunga na CCM baada ya
kukihama chama hicho. |
![]() |
|
Baadhi ya
wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM,
Bi. Samia Suluhu.
Mgombea Mwenza
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu amesema Serikali
itakayoundwa na chama hicho endapo itashika dola katika Uchaguzi Okuu wa
Oktoba, 2015 itahakikisha inapima ardhi yote ya vijiji pamoja na kuainisha
mipaka ili kukomesha migogoro ya ardhi.
Bi. Suluhu
ametoa kauli hiyo alipokuwa akinadi ilaya ya CCM katika Majimbo mawili tofauti
ya Kongwa na Chilonwa Mkoa wa Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za
kufanya kampeni kuwashawishi Watanzania waweze kuipa ridhaa tena Chama Cha
Mapinduzi ili kiunde Serikali na kuwatyumikia wananchi.
Mgombea huyo
mwenza wa urais akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata
ya Chilonwa Kijiji cha Nzali alisema Serikali ya CCM kwa kushirikiana na
halmashauri itaipima ardha ya vijiji na kuweka mipata hasa maeneo sugu ya
migogoro kama Kongwa na Kiteto ili kuzuia migogoro na mapigano kwa jamii hizo
mbili.
Alisema mara
baada ya kupima ardhi na kuweka mipaka kati ya maeneo ya wakulima na wafugaji
watahakikisha mipaka hiyo inatambulika na kuheshimiwa na jamii zote mbili ili
kuzuia migogoro na mapigano ambayo yamekuwa na uhasama mkubwa na kupoteza uhai
na mali za raia wasio kuwa na hatia katika maeneo yenye mgogoro...BOFYA HAPA USOME ZAIDI TAARIFA HII.
|








No comments:
Post a Comment