|
Ndege ya
shirika la British Airways imewaka moto wakati ilikua ikijianda kuruka kutoka
uwanja wa ndege wa Las Vegas, nchini Marekani, Jumanne wiki hii. Watu 172
waliokua katika ndege hiyo wameokolewa kwa dharura, ikiwa ni pamoja na watu
saba ambao wamepata majeraha madogo.
Abiria 159
na wafanyakazi 13 wa ndege hiyo, ikiwa ni pamoja na marubani watatu pamoja na
wafanyakazi wengine kumi, kwa mujibu wa shirika la British Airways ndio
waliokua katika ndege hiyo.
Kwa mujibu
wa akaunti ya Twitter ya mamlaka ya uwanja wa ndege wa McCarran, watu saba
miongoni mwa watu waliokua katika ndege hiyo wamepata majeraha madogo.
|
No comments:
Post a Comment