SHERIA YETU:-oma Taarifa ya TCRA juu ya Vipindi wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, September 11, 2015

SHERIA YETU:-oma Taarifa ya TCRA juu ya Vipindi wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015.



 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kutoa taarifa kuwa kuanzia leo tarehe 10 Septemba 2015, na katika kipindi chote cha kampeni za uchaguzi mkuu 2015, watu ambao sio wagombea wa udiwani, ubunge,urais, wasemaji rasmi wa vyama au watu wasioteuliwa na vyama vya siasa kama wawakilishi hawataruhusiwa kushiriki katika vipindi vya moja kwa moja (Live Programmes) vinavyohusu shughuli za uchaguzi vitakavyorushwa na vituo vya utangazaji.

Utaratibu huu unazingatia Kanuni Za Huduma Za Utangazaji (Maudhui),Utangazaji Wa Uchaguzi Wa Vyama Vya Siasa), 2015, Kanuni ya 4 (f), (h),(i),  5(b), (d), (e) and (f).

Hatua hii inachukuliwa na Mamlaka ili kuweka utaratibu mzuri wa kufanya kampeni za uchaguzi ziwe za amani na utulivu.

Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya kituo cha utangazaji kitakacho kwenda kinyume na utaratibu huu..


IMETOLEWA NA: 
Mkurugenzi Mkuu 
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA 
Tarehe, 11/09/2015  



Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.    

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad