LIGI KUU VODACOM TANZANIA:- Leo September 12,2015 imeanza Msimu mpya wa 2015 / 2016 kwa Mechi 7..Haya ndio matokeo ya Mechi hizo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 12, 2015

LIGI KUU VODACOM TANZANIA:- Leo September 12,2015 imeanza Msimu mpya wa 2015 / 2016 kwa Mechi 7..Haya ndio matokeo ya Mechi hizo.

Beki wa Simba SC, Mohammed Hussein 'Tshabalala' akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Sports.

Ligi kuu soka VODACOM  [Vodacom Premier League], Leo September 12,2015 imeanza Msimu mpya wa 2015/16 kwa Mechi 7.

 Wekundu wa Msimbazi ,Simba SC imeanza vyema Ligi baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji African Sports kwenye Uwanja wa Mkwakwani,mjini Tanga.

Shukrani kwake mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Friday Kiiza ‘Diego’ aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 56, akimalizia kwa kichwa krosi maridadi ya Nahodha Mussa Hassan Mgosi.
Wachezaji wa Azm Farid Mussa (katikati) na Mudathir Yahya (kulia) wakishangilia goli la pili la Azam FC kwa staili ya kusujudu.

Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo,September 12,2015, Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Shukrani kwake Farid Mussa aliyefunga bao la ushindi dakika ya 86 baada ya Jeremiah kuisawazishia Prisons dakika ya 60, kufuatia .

Kipre Herman Tchetche kuanza kuifungia Azam FC dakika ya 42.

Jumapili ,September 13,2015 Mabingwa Yanga SC kushuka Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza na Coastal Union.

VPL-LIGI KUU VODACOM - RATIBA/MATOKEO.

Jumamosi Septemba 12,2015.

Ndanda 1  - 1 Mgambo Shooting  (Nang’wanda - Mtwara)

African Sports 0 – 1  Simba SC  (Mkwakwani - Tanga)

Majimaji 1 – 0 JKT Ruvu  (Majimaji - Songea)

Azam FC 2 – 1 Tanzania Prisons  (Azam Complex - Dsm)

Stand United 0 – 1 Mtibwa Sugar  (Kambarage - Shinyanga)

Toto Africans 1 – 0 Mwadui  (CCM Kirumba - Mwanza),

Mbeya City 0 – 1 Kagera Sugar  (Sokoine - Mbeya)

Jumapili Septemba 13,2015.

Yanga v Coastal Union (Taifa – Dar es salaam).


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.   


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad