KAMPENI ZA UKAWA 2015:- LOWASSA atua Kigoma Jana September 04,2015…. Tizama Kilichotokea huku akibainisha vipaumbele vyake Akichaguliwa na Watanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 05, 2015

KAMPENI ZA UKAWA 2015:- LOWASSA atua Kigoma Jana September 04,2015…. Tizama Kilichotokea huku akibainisha vipaumbele vyake Akichaguliwa na Watanzania.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasalimia wananchi wa Kigoma Kusini, waliokuwa wamefurika kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika jana Septemba 4, 2015.Picha na Othman Michuzi, Kigoma.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, jana Septemba 4, 2015.Picha na Othman Michuzi, Kigoma.


Katika mkutano huo wa Kampeni za UKAWA 2015,Mgombea wa urais ,Bw. Edward Lowassa amebainisha vipaumbele vyake iwapo wananchi watampigia kura ya NDIYO kwa kuhakikisha elimu ya awali hadi chuo kikuu inatolewa bure bila kuwepo kwa michango kwa mwananchi.



Pia amesema katika utawala wake atahakikisha kuwa wakulima wanaondolewa ushuru pamoja na vikwazo vya kuuza mazao nje ya nchi sambamba na kuhakikisha anaongeza ajira kwa vijana mkoani humo kwa kuweka viwanda vya kusindika mafuta ya mawese,sambamba na serikali yake itatunga sera kuhakikisha nyumba za nyasi zinaondolewa nchi nzima na wananchi wanakuwa na makazi bora.

Baadhi ya wananchi wa Mji wa Kigoma Kusini, wakionyesha furaha yako kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,wakati wa Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, Jana Septemba 4, 2015.Picha na Othman Michuzi, Kigoma.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akikaribishwa na Mwenyeji wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo, jana Septemba 4, 2015.Katikati ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe. Picha na Othman Michuzi, Kigoma.








Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokea saluti kutoka kwa Askari Polisi, wakati alipowasili kwa Helkopta, kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, Jimbo la Kigoma Kusini, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo, jana Septemba 4, 2015.Picha na Othman Michuzi, Kigoma.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad