WAUUZA UMEME NURU/SOLAR POWER PANELS' FEKI:- Kukiona cha Moto kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, September 04, 2015

WAUUZA UMEME NURU/SOLAR POWER PANELS' FEKI:- Kukiona cha Moto kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS)

Katibu  Mtendaji wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA), Mhandisi Mathew, akiwaonesha wanahabari Leo September 04,2015,asubuhi Solar Power panels zinazotakiwa kuwa kwenye soko ambazo ni bora.

Katibu  Mtendaji wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA), Mhandisi Mathew Matimbwi (katikati), akiwaonesha wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi Umeme Nuru (Solar Power panels) ambazo hazina ubora zilizokamatwa zikiwa katika soko la Tanzania baada ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Taasisi hiyo, kufanya uchunguzi na kubaini kuwepo katika soko solar hizo. Kulia ni Ofisa Viwango wa TBS, Henry Massawe  na Ofisa Uhusiano, Roida Andusamile.

Ofisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Ubungo Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu shirika hilo kuanza msako mkali wa kuwabaini wafanyabiashara wanaouza Umeme Nuru (Solar Power Panels), zilizochini ya kiwango. Kulia ni  Ofisa Viwango wa TBS, Henry Massawe na Ofisa Udhibiti Ubora wa TBS, Ashura Katunzi.

SHIRIKA  la viwango Tanzania limekuwa likifanya ukaguziwa kushtukiza  wa bidhaa zilizopo sokoni na viwandani mara kwa mara, lengo likiwa niku hakikisha kuwa bidhaa hizo zinakidhi matakwa ya kiwango cha bidhaa husika wakatiwote.

TBS kwakushirikiana naTaasisya NishatiJadididu (TAREA) iliamua kufanya ukaguzi wa kushtukiza kufuatia malalamiko mengi kuhusiana na ubora waVipande vya umeme nuru katika soko la Tanzania na Jumla ya vipande vya umemenuru 1321 kutokaduka na ghala la Regal Solar Ltd vilizuiwa kuuzwa; na 164 kutokaduka la Nishati Electronics Ltd pia vilizuiwa kuuzwa baada ya ubora wake kutiliwashaka mpaka matokeo ya maabara yatakapotoka....BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI JUU YA UKAGUZI HUO.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad