![]() |
|
Akizungumza na waandishi wa habari Jana September
18,2015, jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Ngome Kawe, Mwanasheria wa
Chadema, John Malya amesema “CCM imekuwa ikivunja sheria za uchaguzi kila siku
bila kuchukuliwa hatua yoyote na mamlaka husika, wanatumia nembo za Chadema
ambazo zimesajiliwa na kujulikana.”
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari..’Ndugu waandishi wa habari tumewaita hapa hususani mambo ya
kisheria yanayoendelea kwenye kampeni zoezi la uchaguzi ni zoezi la kikatiba,
sheria ya uchaguzi wa taifa mwaka 1985 kanuni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na
maadili ya uchaguzi wa Ubunge, Urais na Udiwani pamoja na sheria nyingine
ikiwemo ya rushwa na sheria ya vyama vya kisiasa – John Mallya..
|
![]() |
|
‘Sheria kwa mfano ambayo ni maadili ya Uchaguzi ya mwaka huu
vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huu kupitia makatibu wake wakuu
wameweka sign zao inakataza kwa mfano suala la mtu kutoa bango la mtu mwingine
lakini chadema imepata hiyo changamoto kwamba mabango yake wameondolewa kwa
mfano hili bango lipo Nyerere Road pale Mwanza limeondolewa na watu wa CCM
ilikuwa ni nyumbani ya mtu binafsi wakamtishia watachoma nyumbani yake
wakamrushia mawe wakavunja vioo vyake na baada wakaliondoa‘ – John
Mallya..
|
![]() |
|
|
![]() |
|
‘Mabango, sera, vipeperushi vyote vinakuwa
vimesajili na tume ya Uchaguzi kwa madhumuni ya Kampeni kwa mfano ujumbe wa Mabadiliko umesajiliwa na nembo ya CHADEMA
pia imesajiliwa, sasa CCM wanakiuka sheria wame ku copy na ku paste
wanachukua ilani na sera zetu ambapo wamechukua nembo yetu M4C ambayo sisi
tunaita Movement 4 Change huku CCM wakiwa wanasema M4C ni Magufuli 4 Change‘
– John Mallya.
|
![]() |
|
Waandishi wa Habari./Habari kwa hisani ya Millardayo.
Unaweza uka bonyeza HAPA kumsikiliza John Mallya. Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. |











No comments:
Post a Comment