KAMPENI CCM 2015:- Tazama Picha Dr Magufuli akipokelewa kwa kishindo Mjini Bukoba September 21,2015 na kuahidi kuboresha bei ya zao la Kahawa na kuimarisha usafiri katika ziwa Victoria. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 22, 2015

KAMPENI CCM 2015:- Tazama Picha Dr Magufuli akipokelewa kwa kishindo Mjini Bukoba September 21,2015 na kuahidi kuboresha bei ya zao la Kahawa na kuimarisha usafiri katika ziwa Victoria.

Mgombea Urais wa wa Jamhuri ya Muunganano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe magufuli akiwahutubia wakazi wa Bukoba mjini kwenye kutano wa hadhara wa kampeni uliofamyika katika uwanja wa Gymkhana Bukoba mkoani Kagera kumsikiliza Dkt -John Pombe Magufuli..PICHA NA MICHUZI JR-BUKOBA

Katika mkutano huo wa Kampeni uliofanyika jana September 21,2015, Dr John Pombe Magufuli  aliahidi kuimarisha bei ya zao la kahawa ili kuinua uchumi wa Mkoa wa Kagera kutokana na zao hilo kuwategemeo la kibiasahara  sambamba na kuboresha usafiri wa majini katika ziwa Victoria. 

Pia mgombea huyo wa nafasi ya Urais kupitia CCM,Dr John Pombe Mgufuli ambaye alifanya mikutano ya kampeni katika maeneo ya Muleba, Nshamba, Kamachumu, Kemondo, Bukoba vijijini na hatimae Bukoba mjini amewaambia wakazi wa mkoa huo kuwa baada ya serikali kuimarisha mtandao wa barabara kutoka Bukoba hadi Dar es Salaam na nchi jirani, awamu ya tano imejipanga kuimarisha usafiri katika ziwa Victoria ambapo meli mbili zitanunuliwa.

Aidha Dr Magufuli ameonesha kushangazwa na kauli zinazotolewa na waliokuwa viongozi waandamizi wa serikali kuwa serikali haijafanya lolote na kuongeza kuwa viongozi hao wanapaswa kuwaomba radhi watanzania. 
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Balozi Hamis Kagasheki akiwahutubia wananchi wa Bukoba na vitongoji vyake waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni wa Urais,ambapo Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia jioni ya leo mkoani Kagera. 
Wakazi wa Runazi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM alipokuwa akiwahutubia wananchi wilayani Muleba mkoani Kagera jioni ya hapo Jana September 21,2015.
Wakazi wa kijiji cha Nshamba wilayani Muleba wakimsilikiza mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa.

Wakazi wa kijiji cha Nshamba wilayani Muleba wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kufunga barabara wakitaka kusikilizwa shida zao, alipokuwa akiwasili eneo hilo na kuwasalimia Magufuli alipokuwa
 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwapungia wakazi wa Bukoba mjini alipokuwa akiwasili  kwenye viwanja vya Gymkhana mkoani Kagera,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. 
Sehemu ya wananchi wa mji wa Bukoba waliohudhuria leo katika viwanja vya Gymkhana Bukoba mkoani Kagera wakimsikiliza Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Sehemu ya wananchi wa mji wa Bukoba waliohudhuria leo katika viwanja vya Gymkhana Bukoba mkoani Kagera wakimsikiliza Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni... PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad