KAMPENI CCM 2015:-Dk. John Magufuli aahidi kurejesha uchumi wa Mkoa wa Tabora. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 15, 2015

KAMPENI CCM 2015:-Dk. John Magufuli aahidi kurejesha uchumi wa Mkoa wa Tabora.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa mji wa Tabora waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Ali Hassa Mwinyi mapema September 14,2015 ,alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa tabora mjini na kuwaambia kuwa Dk. Magufuli ni kiongozi sahihi anayehitajika Tanzania kwa sasa na kuwataka wananchi kumpigia kura zote ifikapo Oktoba 25 mwaka huu 2015, na kusema kuwa  endapo watanzania watakipa Chama cha Mapinduzi ridhaa ya kuendelea kuliongoza taifa la Tanzania kitaangalia upya baadhi ya sheria kandamizi na kero kwa wananchi na kuzipeleka bungeni ili kuzifuta sambamba na kuondokana na utaratibu wa kuwahamisha watendaji wanaofanya makosa kutoka sehemo moja kwenda nyingine ili kuboresha utoaji wa huduma kwa watanzania waweze kuwa na maisha ya furaha katika nchi yao.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa  wananchi wa mji wa Tabora waliojazana kusikiliza Sera na Mipango ya Chama Cha Mapinduzi itakayotumika kuongoza kwa miaka 10 ijayo, pamoja na mambo mengine ameanisha kero kadha wa kadha ambazo anataka kuzivalia njuga akiwa madarakani ikiwa ni pamoja na kuzuia unyanyasaji kwa wananchi wa hali ya chini lakini pia akaahidi kurejesha uchumi wa Tabora kwa zao la tumbaku pamoja na kuimarisha reli.

Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ndani ya uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora..PICHA NA MICHUZI JR-TABORA.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad