|
Kampuni ya
Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, ambayo ni mdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya mpira
wa miguu Tanzania bara leo imekabbidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo
yenye thamani ya shilingi milioni 490,00,000.
Akikabidhi
vifaa hivyo leo Semptember 02,2015 jijini Dar es salaam, Mkuu wa Kitengo cha
Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twisa alsiema kuwa kwa mara nyingine
tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri Vodacom inakidhi
vifaa mbalimbali vy a ligi ambavyo ni jezi za kawaida, jezi za mechi, viatu na
vifaa vingine vinayohitajika.
“Tunajisikia
furaha kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwaa tunatekeleza matakwa ya mkataba
wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki lii zimejiandaa vya
kutosha kwa msimu mpya 2015/2016” Alisema Twissa.
Twissa
alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo
unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda kuona
wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake wanapata buruddaniya mchezo waupendao
pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa duniani kote, ikiendelezwa
inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na taifa kunufaika kwa mapato makubwa
ya kodi kutoka sekta hii.
Aliwataka
wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha zaidi ligi ya Tanzania na kuongeza
maslahi kwa wachezaji wanaoshiri katika ligi “Tukiunganisha nguvu timu zetu
zinaweza kuwa na wachezaji wa kimataifa pia ni muhimu kwa wadau mbalimbali
kuanza kuwekeza katika timu za vijana chipukizi kwa kuwa vipaji vinaanza ngazi
ya chini ambako vinapaswa kuibuliwa na kuendelezwa” Alisema Twissa.
Naye Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura aliishukuru Kampuni ya Vodacom
na kuvitaka vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya Vodacom kuheshimu chapa ya
mdhamini wakati wote wa ligi.
“Ninatoa
mwito kwa vilabu vyote kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini katika kuhakikisha
ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa” alisema.
Aliongeza
kuwa TFF isingependa kutumia kanuni na sharia kuadhibu klabu inayokwenda
kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya madhamini kama ambavyo
anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa.
Alisema ligi
ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na maandalizi yote kukamilika mapema pia
timu zitakazoshiriki zimejiandaa vya kutosha kuhakikisha ligi inakuwa na
msisimko na ushindani mkubwa.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment