Mwenyekiti
wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Mhe Samia Suluhu
Hassan, Mgombea mwenza wa ugombea Urais kwa tiketi ya Chama hicho tawala
Dkt John Pombe Magufuli leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es salaam.
Mgombea
Urais kwa tiketi ya CCM tawala Dkt John Pombe Magufuli akiongea na
wazee wa Dar es salaam leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es salaam.
Meza
Kuu ikimfurahia Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM tawala Dkt John Pombe
Magufuli akiongea na wazee wa Dar es salaam leo Agosti 19, 2015 katika
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa Wazee wa CCM wa Dar es salaam akipeana mikono na Mgombea Urais kwa
tiketi ya CCM tawala Dkt John Pombe Magufuli baada ya kuongea na wazee
wa Dar es salaam leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

PICHA NA IKULU.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi
taifa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete
amesema mchakato wa uteuzi wa mgombea wa nafasi ya urais wa Tanzania Dr John
Pombe Magufuli umedhihirisha kuwa chama hicho hakiteuwi kada ama mwanachama
yeyote kutokana na fedha zake na kwamba uteuzi wake umetokana na mapenzi ya
mungu kwa Tanzania kumpata mtu atakayesimamia kwa dhati rasilimali za taifa na
kuwatumikia wanyonge na asiyeyumbishwa na rushwa.
Akizungumza na wanaccm mkoa wa Dar
es Salaam Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi taifa na rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete amewahakkishia wanaccm wote
nchini kuwa chama hicho kina mgombea mzuri tena mzuri sana katika kila hali iwe
na ya ucha mungu, uwajibikaji na uchapakazi kwa kuzingatia misingi ya haki na
hana kigugumizi katika utendaji wake na kwamba ni mpango wa mungu Tanzania
kumpata kiongozi mwadilifu atakayesimamia uwajibikaji na uadilifu na kwamba ni
mtu asiyejikweza na kwamba ni mgombea wa sampuli nyingine.
Akielezea sifa za Dr John Pombe
Magufuli mwenyekiti huyo wa CCM taifa na rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete amesema Dr Magufuli anachukia sana uzembe,
rushwa na ubabaishaji lakini pia usawa wa kijinsia na ndo maana akamteuwa
mgombea mweza kuwa mwanamke.
Mgombea wa kiti cha urais kupitia
CCM Dr John Pombe Magufuli akizungumza na wanaccm hao wa mkoa wa Dar es Salaam
amesema Tanzania ni nchi ya amani ambayo inapaswa kuendelezwa kwa misingi ya
amani bila ukabila na ukanda wala ubaguzi wa aina yeyote na kuwataka watanzania
kuendelea kuwa wamoja na kuwahakikishia watanzania kuwa anatosha katika kutatua
kero mbalimbali za mtanzania wa kawaida na makundi mbalimbali.
Awali, akizungumza na wanaccm mkoa
wa Dar es Salaam, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni
mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM mikoa Ramadhani Madabida amesema mkutano huo ni
wa kwanza tangu kumalizika kwa vikao vya uchujaji wa wagombea katika ngazi zote
vilivyoongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Dr Jakaya Kikwete na kumhakikishia
kuwa wanaccm wa mkoa wa Dar es Salaam wako imara na kwamba wako tayari kwa
mapambano ya kisiasa.
Katika tukio jingine, mapema
asubuhi, Dr John Pombe Magufuli akiambatana na mgombea mwenza mama Samia Hassan
Suluhu walirejesha na kusaini fomu za tume ya taifa ya uchaguzi katika mahakama
kuu ya Tanzania kwa mujibu wa taratibu na sheria ya tume hiyo ya taifa ya
uchaguzi ambapo kwa mujibu wa kanuni na taratibu za tume hiyo wagombea wote
wanahitaji kupata wadhamini wasiopungua mia mbili katika baadhi ya mikoa
ikiwemo visiwa vya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment