Mashua
zenye tanga zinazojaza upepo zikichanja mbuga katika mawimbi makali
kwenye bahari ya hindi kwenye fukwe za Yatch Club wakati wa mashindano
ya mbio za Mashua za Mercedes Benz Cup 2015 yaliyodhaminiwa na kampuni
ya CFAO Motors kwa miaka 9 sasa, yaliyomalizika mwishoni mwa juma jijini
Dar es Salaam.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
KLABU
ya Yatch ya Dar es salaam iliyopo Msasani jijini Dar es salaam
inatafuta fedha kuwezesha washiriki wake wanne katika mbio za mashua za
kisasa kwenda kushiriki michezo ya All Africa games itakayofanyika
baadae mwaka huu.
Kauli
hiyo imetolewa katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya
kumalizika kwa patashika ya siku mbili ya mbio za mashua za kisasa
zinazosukumwa na matanga yanayopokea upepo na zile ambazo hazina.
Mbio
hizo ambazo zimedhaminiwa na CFAO Motors kupitia bidhaa yake ya
Mercedes Benz Cup 2015 zilishirikisha watu 30 wakiwa ndani ya mashua 15
za aina tofauti.
Ofisa
mmoja wa klabu hiyo Andrew Bogd alisema kwamba ushiriki wa watanzania
katika mashindano ya kimataifa hautakuwa wa kwanza kwani wameshashiriki
katika mchezo hiyo Afrika Kusini na Morocco mwaka jana.
Alikuwa
akizungumzia mafanikio ya klabu hiyo katika kuufanya mchezo huo
kujulikana kwa wazawa wa Tanzania ambao wanapenda michezo ya katika maji
hasa ya kukimbiza mashua.
Katika
mbio hizo ambapo kulikuwa na washindi takribani zaidi ya saba kwa
kuzingatia daraja mshindi wa mashua zenye tanga inayojaza upepo alikuwa
Al Bush akishirikiana na Robert Fine. Mshindi wa Pili wa ngazi hiyo
alikuwa Michael Sulzer aliyekuwa katika mashua na Andreas Schmidt na
ushindi wa tatu ulikwenda Roland Van de Ven akiwa na Peter Scheren.
Washiriki
wakipambana na mawimbi wakati wa mashindano ya mbio za mashua za
Mercedes Benz Cup 2015 yaliyomalizika mwishoni mwa juma jijini Dar.
Washindi
hao walikabidhiwa tuzo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric
Potin ambaye safari hii katika udhamini wao walikuwa wanatangaza gari la
Mercedes GL –CLASS.
Washindi
wengine katika kategori ya mashua za kisasa za kawaida walikuwa Andrew
Boyd akiwa na Max Pennan Kok wakati washindi wa pili walikuwa David
Scott akiwa na Cassie Dietliefs na washindi wa tatu walikuwa Cyrille
Girardin na Gemma Quickenden.
Mercedes
Benz ambao wanadhamini mashindano mbalimbali ya mashua za kisasa za
ngazi mbalimbali duniani, wamekuwa wakidhamini michuano hiyo ya Dar es
salaam kwa mara ya 9 sasa.
Msemaji
wa Yatch Club, Bogd akizungumzia michuano hiyo iliyokuwa ya siku mbili
alisema iliyiojaa changamoto kubwa hasa siku ya kwanza ambapo mabahari
walioonesha umahiri kukabiliana na upepo mkali na kuongoza mashua zao
katika muda waliopaswa kuufikia wakishindana katika mfumo wa juu hadi
chini au kwenda kwa mfumo wa pembetatu.
Siku ya kwanza ya mbio hizo Jumamosi upepo ulivuma kwa kasi ya noti 20 kwa saa.
“
…haikuwa kazi rahisi siku ya kwanza. Lakini hiyo ndio raha ya mchezo
huu.Bahari inapokuwa ‘ngumu’ ambapo waendesha mashua hao ni kama vile
wanataka kutemwa kutoka kwenye mashua, hivyo wakilazimika kutumia
maarifa yao kuidhibiti, ndio raha ya mchexzo wenywe” alisema Bogd.
Mshindi
wa mashua zenye tanga inayojaza upepo Al Bush akishirikiana na Robert
Fine wakirejea katika fukwe za Yatch Club jijini Dar es Salaam wakati wa
mashindano hayo ya mbio za Mashua za Mercedes Benz yaliyodhaminiwa na
Kampuni ya CFAO Motors kupitia bidhaa ya Mercedes Benz Cup 2015 mwishoni
mwa juma jijini Dar es Salaam.
Washiriki walilazimika kufanya hatua saba za mbio hizo ambapo kila hatua ilikuwa ni dakika 40.
Pamoja
na washiriki hao kupewa zawadi ofisa huyo alitaka watu zaidi kushiriki
katika mashindano hayo ambayo kwa jinsi siku zinavyoenda watanzania
wengi zaidi wanafika kujifunza mashindano hayo ambayo yanahitaji maarifa
na pia kuzingatia usalama kwa kutumia mashua za kisasa za aina tofauti.
Katika mashindano hayo huwa kunakuwa na mashua kubwa na nyingine za kati na ndogo.
Aidha
alisema kwamba wanaanzaa kufundisha mchezo huo kuanzia miaka minane na
kwamba huwezi kufundisha udhibtii wa mashua kwa mtu mzima kwani kuna
hatua mbalimbali zinazojenga uzoefu wa mchezo wenyewe.
Alisema
watoto ambao sasa wameshapita umri wa kuendesha mashua za kati
wameshaanza kushiriki na kwamba wanatoa changamoto kubwa kwa washiriki
wenye umri mkubwa katika mchezo huo.
Dar
es Salaam Yacht Club ambayo hufanya mashindano ya mashua ya kisasa
zikiwemo catamaran, Cadets, yachts na Lasers ilianzishwa mwaka 1933
katika bandari ya Dar es salaam, mwaka 1967 ilihamishiwa ilipo sasa la
Leopard’s Cove, ghuba ya Msasani.
Panmoja na kufanya shughuli za mbio za mashua pia wana bwawa la kuogelea, baa na mgahawa.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric Potin aliyeipa mgongo 'camera'
akijaliana jambo na Mkurugenzi wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani
(aliyesimama kushoto katikati) pamoja na Meneja Masoko wa CFAO Motors,
Shekha Said. Wengine ni maofisa wa Yatch Club jijini Dar, kabla ya zoezi
la kukabidhi vikombe na zawadi kwa washiriki.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric Potin (kushoto) akikabidhi kikombe
kwa washindi wa kwanza wa mashindano ya Mercedes Benz Cup 2015, Al Bush
aliyeshirikiana na Robert Fine, huku Mkurugenzi wa fedha wa CFAO
Motors, Aldo Pagani akishuhudia tukio hilo.
Washindi
wa Mercedes Benz Cup 2015, Al Bush, Robert Fine waliosindikizwa na
Andrew Boyd wa Yatch Clup (wa pili kushoto) pamoja na Max Pennan Kok
wakifurahia kikombe chao katika picha ya pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu
wa CFAO Motors, Eric Potin (kushoto) na Mkurugenzi wa fedha wa CFAO
Motors, Aldo Pagani (kulia).
Washindi
wa Mercedes Benz Cup 2015, Al Bush, Robert Fine katika picha ya pamoja
na Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric Potin (kushoto), Mkurugenzi
wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani (wa tatu kulia), Meneja Masoko wa
CFFAO Motors, Shekha Said (wa pili kulia) pamoja na Meneja Mauzo wa
matairi CFAO Motors, Pietre Van Eeden (kulia).
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric Potin akimpongeza mchezaji wa
mashindano ya mbio za mashua za Mercedes Benz Cup 2015, Michael Sulzer
kwa ushiriki wake.
Mshindi
mdogo kuliko wote wa mashua za kawaida shindano la Mercedes Benz Cup
2015, Casey Dietliefs (katikati) aliyeshirikiana na David Scott
(kushoto) wakipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa fedha wa CFAO
Motors, Aldo Pagani (kulia).
Mkurugenzi
wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani (kulia) akisaidiwa na Mwenyekiti
wa Dar Yatch Club, Brian Grant wakati akikata utepe kuzindua gari
iliyotolewa na kampuni ya CFAO Motors kwa Dar Yatch Club kama shukrani
ya ushirikiano baina ya CFAO Motors na Dar Yatch Club.
Mkurugenzi
wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani na Meneja Masoko wa CFAO Motors,
kwa pamoja wakizindua gari hiyo wakati wa mashindano ya Mercedes Benz
Cup 2015.
Mwenyekiti wa Dar Yatch Club, Brian Grant akiwasha gari hiyo kuashiria uzinduzi rasmi.
Mmoja
wa wananchama wa Yatch Club akiangalia gari aina ya Mercedes Benz GL
Class iliyowekwa katika viwanja vya Yatch Club kama nembo ya udhamini wa
mashindano ya mbio za mashua za Mercedes Benz.
Pichani
juu na chini ni washiriki wa mashindano ya mbio za mashua za Mercedes
Benz na familia zao wakisubiri zoezi la kukabidhiwa zawadi na vikombe
kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo CFAO Motors mwishoni mwa juma.
Washiriki wa mashindano ya mashua ya Mercedes Benz Cup 2015 katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment