MBIO ZA URAIS TANZANIA 2015:- Taswira Picha wakati Mchungaji Mtikila wa DP, Fahmi Dovutwa wa UPDP, Bw.Maxmilian Lyimo wa TLP Wachukua Fomu za Uteuzi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 01, 2015

MBIO ZA URAIS TANZANIA 2015:- Taswira Picha wakati Mchungaji Mtikila wa DP, Fahmi Dovutwa wa UPDP, Bw.Maxmilian Lyimo wa TLP Wachukua Fomu za Uteuzi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC.

 Mgombea kiti cha urais kupitia TLP, Maxmillian Lyimo, akionyesha mkoba wenye fomu za uteuzi za tume ya taifa ya uchaguzi, NEC, baada ya kukabidhiwa Leo Agosti 01,2015 na tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania -NEC....PICHA NA K-VIS BLOG.

Mgombea kiti cha Urais kupitia TLP, Maxmillian Lyimo, (kulia), akipokea mkoba wenye fomu za uteuzi wa kuwania kiti cha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015, (kulia), za Tume hya Taifa ya Uchaguzi, (NEC), kutoka kwa afisa mwandamizi wa tume hiyo, makao makuu ya NEC, jijini Dar es Salaam leo asubuhi Jumamosi Agosti 1, 2015.
Mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa, (kulia), akipokea mkoba wenye fomu za uteuzi wa kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015, za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, (NEC), kutoka kwa afisa mwandamizi wa tume hiyo, makao makuu ya NEC, jijini Dar es Salaam leo asubuhi Jumamosi Agosti 1, 2015. 

Dovutwa amekuwa mgombea wa kwanza kuchukua fomu hizo na kazi iliyo mbele yake ni kutafuta wadhamini 200 ambao ni raia wa Tanzania wenye shahada za kujiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi huo. Dovutwa alifuatana na mgombea mwenza wake, Hamad Mohammed UIbrahim na wanachama wachache wa chama hicho.
MGOMBEA wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, akikabidhiwa fomu za uteuzi za tume ya taifa ya uchaguzi, NEC, kutoka kwa afisa uchaguzi mwandamizi wa tume hiyo, makao makuu ya NEC jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Agosti 1, 2015.
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad