MBIO ZA URAIS TANZANIA 2015:-Lowassa arejesha fomu, wanachama 1.6 milioni wamdhamini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 01, 2015

MBIO ZA URAIS TANZANIA 2015:-Lowassa arejesha fomu, wanachama 1.6 milioni wamdhamini.

Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiwasalimia  maelfu ya wafuasi na wapenzi wa Chama hicho kwa ishara ya vidole viwili, wakati alipowasili kwenye Ofisi ya Makao Makuu ya Chama hicho, Kinondoni Jijini Dar es Salaam jioni ya leo Agosti 01,2015. 

Mh. Lowassa alifika ofisini hapo kurudisha fomu za kuomba ridhaa ya Chama hicho, kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu 2015.


Mkurugeni wa Oganaizesheni na Uratibu wa Kanda wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Benson Kigaila akionyesha fomu zenye idadi ya wananchi waliomdhani Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama hicho, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa, ambapo jumla ya wananchi 1,662,397 walijitokea katika maeneo mbali mbali kumdhamini Mgombea huyo.

Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa (wa pili kulia) akikabidhi fomu hizo kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Prof. Abdalaah Safari wakati wa hafla fupi ya kurudisha fomu hizo, iliyofanyika jioni ya leo Agosti 01,2015 kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA, Kinondoni Jijini Dar es salaam. 

Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Wadhamini wa CHADEMA, Mh. Arcado Ntagazwa na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA - Zanzibar, Salum Mwalim.

Sehemu ya Viongozi wa CHADEMA waliokuwepo kwenye hafla hiyo.

Baadhi ya Wadau walioambatana na Mh. Lowassa…. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.

HATIMAYE Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa leo Agosti 01,2015 amerejesha fomu ya kuomba uteuzi kuomba urais kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). 

 Aidha, katika urejeshaji wa fomu Lowassa amepata udhamini kutoka mikoa 32 ambao amedhaminiwa na wanachama zaidi ya milioni 1.6

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Organaizesheni na Uchaguzi, Benson Kigaila amesema, wadhamini hao wamepatikana kutoka katika Kanda 10 na Mikoa 32 kwa nchi nzima.

Sasa safari ya matumaini kupitia CCM imeishia njiani,safari ya uhakika kupitia Chadema imefika na kipindi hiki lazima kieleweke na tunaenda kuiondoa CCM madarakani asubuhi kweupe”,amesema Kigaila.

Ameongeza kuwa wanachama kutoka mikoa yote walikuwa wakitamani Lowassa apitie mikoa yote ili kumdhamini kutokana na muda mchache wameamua kumdhamini kupitia njia ya simu.

Kigaila ambae pia ni Mkurugenzi wa Kanda wa Mambo ya Uchaguzi wa chama hicho amesema wanachama wasijali chochote kwa kuwa baada ya mkutano mkuu kumpitisha mgombea ambao unatarajia kufanyika Agosti nne atachanja mbuga kuzunguka mikoa yote.

Nae Profesa Abdallah Safari ambae ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara amesema amemshukuru Lowassa kwa kurejesha fomu hiyo kwa kuwa baadhi ya watu walidhani angeingia mitini kwa hiyo sasa tunajiandaa kwenda kuchukua dola.

Nae Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu amesema chama tawala hawawezi kuwasambaratisha chadema na kuja kwa Lowassa ni mpango wa mungu na nyama zote walizopanga hazitafanikiwa.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad