Muonekano wa barabara ya Tunduma- Sumbawanga ambapo Barabara hiyo sasa imekamilika. |
Wakati
wakandarasi walipokuwa wanajenga daraja hili katika eneo la Miangalua kwenye
barabara ya Tunduma-Sumbawanga mwaka 2011 ambapo Barabara hiyo sasa imekamilika.
|
Barabara ya
Mwanza-Musoma iko katika hali nzuri.
|
Ujenzi wa
barabara ukiendelea katika baadhi ya miradi nchini.
|
UJENZI WA BARABARA- Ujenzi wa barabara ya Iringa-Dodoma umekamilika kwa asilimia 95, bado
maeneo machache tu likiwemo hili la Mlima Nyang'oro ambapo Wachina wameuchonga
ili kupunguza kona katika umbali wa kilometa 15. (Picha zote na Daniel Mbega
wa www.brotherdanny.com).
Katika kipindi cha uongozi wa
Serikali ya awamu ya nne, barabara zenye urefu wa jumla ya 6,276.82km
zimejengwa kwa gharama ya Dola
102,654.98 milioni, nyingi kati ya hizo zikiwa za lami na hivyo
kuutengeneza mtandao imara wa miundombinu ya barabara.
Kujengwa kwa barabara hizo
kumerahisisha hata usafiri ambapo leo hii magari ya abiria na mizigo kutoka Dar
es Salaam kwenda Musoma, Mwanza, Kagera na Kigoma hayahitaji kuzunguka Nairobi
bali yanakwenda moja kwa moja.
Hivi sasa usafiri wa kutoka Dar es
Salaam kwenda Sumbawanga ni wa siku moja badala ya siku mbili, kama ilivyo kwa
usafiri wa Dar es Salaam kwenda Mbinga, jambo ambalo miaka 10 iliyopita
lilikuwa ndoto.
Asilimia 90 ya miradi hiyo
imesimamiwa na Dk. Magufuli akiwa Waziri wa Miundombinu katika kipindi cha
mwaka 2010 hadi 2015na bado miradi mingine inaendelea kujengwa japo imesimama
kidogo kutokana na ufinyu wa bajeti.
Kampuni za Kichina zimepata mikataba
mingi ya ujenzi. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wakala wa Barabara nchini
(TANROADS), katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, kampuni 14 kutoka China
zimeingia jumla ya mikataba 58 ya ujenzi wa kilometa 3,140.85 yenye thamani ya
Dola 1.75 bilioni.
Kampuni ya China Henan International
Cooperation Group Co., Ltd. (CHICO) ambayo ilipata mkataba wenye thamani ya
Dola 206 milioni kutoka Wakala wa Barabara Zambia kujenga barabara ya
Mansa-Luwingu yenye urefu wa kilometa 175, peke yake imeingia mikataba 13
nchini Tanzania ya barabara zenye urefu wa kilometa 705.2 zikiwa na thamani ya
Dola 490.26 milioni.
Hizi ni pamoja na barabara za
Singida-Iguguno (76km) yenye thamani ya Dola 20.55 milioni; Sekenke-Shelui
(33km) yenye thamani ya Dola 12.51 milioni; Mwandiga-Manyovu (60km) wenye
thamani ya Dola 32.54 milioni; Kigoma-Kidahwe (35.7km) kwa Dola 19.56 milioni;
Bonga-Babati (19.20km) kwa Dola 11.95 milioni; Tabora-Urambo (42km) kwa Dola
31.17 milioni; Kyaka-Bugene (59.1km) kwa Dola 51.6 milioni; Dareda-Minjingu
(84.6km) kwa Dola 51.6 milioni); Kidahwe-Uvinza-Ilunde (76.6km) kwa Dola 47.5
milioni; Isaka-Ushirombo (132km) kwa Dola 88.223 milioni; Kilwa Road Phase III
(1.5km) kwa Dola 3.4 milioni; Nyanguse-Musoma (85.5km) kwa Dola 3.3 milioni; na
Kagoma-Lusahunga (154km ) kwa ubia na kampuni ya CRSG kwa gharama ya Dola 116.2
milioni.
China Sichuan International
Cooperation Co., Ltd (SIETCO) inajenga barabara zenye urefu wa 283.9km zenye thamani
ya Dola 123.03 milioni ambazo ni Isuna-Singida (63km) kwa Dola 18.5 milioni;
Tarakea-Rongai-Kamwanga (32km) kwa Dola 8.8 milioni; Iringa-Migori (95.1km) kwa
Dola 51.123 milioni; na Migori-Fufu Escarpment (93.8km) kwa Dola 44.7 milioni,
wakati kampuni ya CICO inajenga barabara ya Nangurukuru-Mbwemkuru yenye 95km
kwa thamani ya Dola 23.82 milioni.
Kampuni ya China Geo-Engineering
Corporation International Ltd (CGC INT'L) inajenga barabara zenye urefu wa
525.9km zikiwa na thamani ya Dola 151.2 milioni. Barabara hizo ni Shelui-Nzega
(112km) kwa Dola 12.6 milioni; Kyamorwa-Buzirayombo (120km) kwa Dola 29.822
milioni; Manyoni-Isuna (54km) kwa Dola 18.4 milioni; Arusha-Namanga (104.2km)
kwa Dola 49.64 milioni; Chalinze-Tanga Phase I (125km ) kwa Dola 25.9 milioni
na ndiyo kampuni iliyojenga Daraja la Mkapa (Daraja la Umoja 10.7km)
linalounganisha Tanzania na Msumbiji kwa gharama ya Dola 14.9 milioni.
Katika orodha hiyo, ipo kampuni
inayomilikiwa na serikali ya China, Hydropower Engineering and Construction Company
(SINOHYDRO) ambayo ilipata mikataba 12 nchini Tanzania ya ujenzi wa barabara
zenye urefu wa jumla ya 779.95km zenye thamani ya Dola 434.36 milioni.
Barabara hizo ni Sengerema-Usagara
(40km) kwa gharama ya Dola 21.724 milioni; Buzirayombo-Geita (100km) kwa Dola
25 milioni; Geita-Sengerema (50km) kwa Dola 24.034 milioni; Dodoma-Mayamaya
(43.65km) kwa Dola 25 milioni; Manyoni-Itigi-Chaya (89.3km) kwa Dola 66.56
milioni; Puge-Tabora (56.1km) kwa Dola 35.085 milioni; Handeni-Mkata (54km) kwa
Dola 34.81 milioni; Korogwe-Handeni (65km) kwa Dola 38.4 milioni; Katesh-Dareda
(73.8km) kwa Dola 38.94 milioni; Singida-Katesh (65.1km) kwa Dola 31.34
milioni; Tanga-Horohoro (65km) kwa Dola 42.43 milioni; na Peramiho
Junction-Mbinga (78km) kwa Dola 48.444 milioni.
CHIKO ilijenga barabara ya Sam
Nujoma jijini Dar es Salaam yenye urefu wa 4km kwa thamani ya Dola 7.9 milioni,
China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) ilipata mikataba minne
ya kujenga barabara zenye urefu wa 145.6km kwa thamani ya Dola 95 milioni.
Barabara hizo ni Magole-Turiani
(48.6km) kwa Dola 25.43 milioni; Tabora-Urambo (52km) kwa Dola 36.3 milioni;
Dumila-Rudewa (45km) kwa Dola 25.5 milioni na Jangwani Depot kwa ajili ya mradi
wa mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam (BRT) kwa Dola 7.81 milioni.
(Imeandaliwa na www.brotherdanny.com. Simu: 0656-331974)
|
No comments:
Post a Comment