MAFANIKIO KAGERA:-Ni kuhusu maambukizo ya Malaria yashuka. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, August 17, 2015

MAFANIKIO KAGERA:-Ni kuhusu maambukizo ya Malaria yashuka.

Kiwango cha maambukizi ya malaria mkoani Kagera umetajwa kushuka tofauti na ilivyokuwa kabla ya unyunyiziaji wa dawa ya ukoko majumbani. 

Mkuu wa mkoa wa Kagera B.wJohn Mongela, (Pichani ) amesema kuwa taarifa ya utafiti wa UKIMWI na MALARIA mwaka 2007, inaonesha kuwa kiwango cha maambukizi ya malaria kwa watoto chini ya miaka mitano kilikuwa asilimia 41, ambapo utafiti 2011 kilishuka hadi asilimia 9 na 2015 utafiti  umeonesha maambukizi yameshuka kutoka 41% hadi 9.5%.

Pamoja na kuipongeza taasisi ya utafiti wa malaria RTI, mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa mikoa tafiti zinaonesha kuwa mikoa mingine ambayo haikuwa na utaratibu wa unyunyiziaji dawa ya mbu majumbani, kiwango cha malaria kimeendelea kuwa juu, akitolea mfano mkoa wa Lindi 35.7 kwa kupunguza kiwango kidogo hadi asilimia 29 kwa mwaka, huku Kigoma maambukizi yakipanda kutoka asilimia 19.6 mwaka 2007 hadi asilimia 26 mwaka 2011.

Mkuu wa mkakati wa unyunyiziaji dawa majumbani nchini Bw.Stephen Magesa, ameiomba ofisi ya mganga mkuu kuongeza nguvu katika vijiji vya kando ya ziwa wilayani Muleba  kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi ya malaria, ingawa tathmini yake bado inafanyika.
Mratibu wa RTI uhamasishaji mkoani Kagera Bw.Deodart Ngaiza, amesema unyunyiziaji wa dawa ya kuua mbu majumbani ulianza mwaka 2007 kwa kushirikisha jamii husika ili kuondoa dhana ya imani potofu iliyokuwa imetawala kuwa zinapunguza nguvu za kiume.

Amewashauri wananchi kuzingatia maelekezo ya wataalamu katika matumizi ya nyumba zilizopuliziwa kutumika sambamba na vyandarua wanavyopewa Mkutano wa wadau wa utekelezaji huduma za afya mkoani Kagera, umefanyika kwa kuwashirikisha wakurugenzi wa halmashauri za mkoa, watendaji wa huduma za afya na waratibu wa mradi wa unyunyiziaji wa dawa ya kuua mbu majumbani mkoa na taifa.



Na Mwanaharakati....BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

 
PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp  +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad