Mwenyekiti wa sasa na Rais wa
Tanzania, Mh Jakaya Kikwete amesema, CCM haikubahatisha kumteua Dk John
Magufuli kuwa mteule wa chama hicho katika urais na kwamba, “tumemweka kwa sifa
zake, tunataka rais anayeipenda nchi na anayependa wananchi wa nchi hii.”
“Magufuli anayo sifa hiyo. Tumesema,
hatutaki kuchukua mgombea mwenye makando kando mengi na tukatumia muda wetu
mwingi kujitetea sisi na yeye kabla ya kuomba kura. Tunamtaka mgombea
mwaminifu, mwadilifu. Safari hii Mungu kamchagua Magufuli.”
Katika
Uzinduzi huo,Viongozi wa Makundi mbalimbali
walipata fursa ya kuhutubia na kueleza hisia
za makundi hayo na miongoni mwa
waliowakilisha ni Mwenyekiti msaidizi wa Machinga mkoa wa Dar es salaam , Mwenyekiti
wa Shirikisho la watu wenye ulemavu Tanzania na Mwenyekiti wa bodaboda mkoa wa Dar es
Salaam.
Pia
Jaji Joseph Sinde Warioba,
amewaeleza watanzania kuhusu sifa za wagombea wa CCM kuwa chama kimetazama sifa
tatu, UCHAPA KAZI, UADILIFU na UZALENDO.
Amesema kuwa ukizungumzia uchapakazi
wa magufuli ni lazima uutazame katika vipindi vitatu alivyoudumu katika wizara
kadhaa hasa ya ujenzi ambayo imeiunganisha Dar es salaam na mikoa yote Tanzania
kwa barabara, akifanya kazi ndani na nje ya serikali.
Amebainisha kwamba, mabadiliko
yanayotajwa na baadhi ya watu tayari yamefanywa na CCM kwa kiasi kikubwa kwa
mara ya kwanza baada ya kuweka wagombea wenye sifa hizo tatu na kubwa zaidi
kumweka mwanamke kama Makamu wa Rais wa Tanzania.
Kwa
Upande wake Mgombea Urais Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Serikali ya mapinduzi
ya Zanziba, Dr.Ali Mohamed Shein,amesema kuwa
ni wakati wa watanzania kuenzi kazi kubwa iliyofanywa na Magufuli, na Wazanzibar
wanayatambua, wakatuma salamu zao ili kudhiilisha ukweli wao, akisisitiza kuwa
uongozi si wa kujaribu ,Hivyo Watanzania wawe makini katika kuchagua October 25,2015.
Rais
mstaafu wa awamu ya pili,Mzee
Ali Assan Mwinyi amesema kuwa upinzani ni muhimu na upo siku nyingi lakini siku
imefika wao kuazima viongozi na dhamira ya waliokwenda wameenda kuongeza nguvu
ili kuishinda CCM lakini yawezekana ikawepo CCM mbili A na B.
Rais wa awamu ya tatu; Mzee Benjamin Willaim Mkapa, amesema katika hao nane
walioteuliwa na tume ya uchaguzi, watanzania watazame timu bora kwa sababu
ndiyo itasukuma maendeleo yao lakini watambue kuwa hapa nchini kuna chama kimo
tu cha ukombozi, huku akikumbusha sifa za viongozi madhubuti kuwa ni wale
wanaotekeleza imani za wananchi kwa vitendo, kushiriki na wenzao, kuwa mstari
wa mbele kutekeleza mambo ya umma kupitia CCM.
|
Sunday, August 23, 2015
Home
SIASA
KAMPENI ZA CCM KITAIFA:- Mamia wajitokeza Leo August 23, 2015 Viwanja vya Jangwani-Dar es Salaam.
KAMPENI ZA CCM KITAIFA:- Mamia wajitokeza Leo August 23, 2015 Viwanja vya Jangwani-Dar es Salaam.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment