KAMPENI ZA CCM 2015:-Dr Magufuli amewautubia wakazi wa katavi na kuwaahidi kutatua kero zao. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, August 24, 2015

KAMPENI ZA CCM 2015:-Dr Magufuli amewautubia wakazi wa katavi na kuwaahidi kutatua kero zao.

Waziri Mkuu MizengO Pinda akimtambulisha Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli mbele ya umati wa watu waliofurika jioni ya leo  August 24, 2015 kwenye uwanja wa Azimio mjini Mpanda mkoani Katavi wakati wa muendelezo wa kampeni za chama hicho mkoani humo… PICHA NA MICHUZI JR-KATAVI.

 Chama cha CCM kimezindua kampeni zake jana August 23, 2015 katika viwanja vya Jangwani jijini Dar na kuhudhuriwa na maelfu ya wanachama na wakereketwa wa chama hicho cha CCM.

Wwataki akimpokea Dr Magufuli ambaye yuko Mkoani humo akiendelea na Kampeni za kuomba ridhaa ya Watanzania ili wamchague awe Rais wa awamu ya Tano wa Tanzania,Waziri Mkuu wa Tanzania,Bw Mizengo Pinda amesema Chama cha Mapinduzi CCM kitapata Ushindi katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu 2015 kwa kuwa kimejipanga vema na kukubalika kwa Mgombea Urais wa CCM Dr John Magufuli.

Sehemu ya umati wa Wananchi wa kata ya Mishamo,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni,wilayani Mpanda mkoani Katavi,ambapo  Dr Magufuli amewondoa hofu na kuwataka kuishi kwa amani na upendo kama walivyo watanzania wengine huku akiwahidi kuwapelekea huduma za msingi za binaadamu ikiwemo maji, umeme, barabara na hospitali.
Dr John Pombe Magufuli (Kushoto ) sambamba na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kulia) amehutubia mikutano mitatu katika maeneo ya makazi ya waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa 1972 ya mishamo kilimomita zaidi 150 kutoka mjini Mpanda, kisha makazi ya katumba na baadae katika mkutano mkubwa wa hadhara mjini Mpanda na kuahidi kuwatatulia kero ya kosefu wa barabara inayosababisha kushindwa kupeleka mazao yao sokoni kutoka katika mikoa ya Katavi, Kigoma na Rukwa kwa kuiunganisha na mikoa mingine ya Tanzania.

Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo mkubwa wa hadhara katika uwanja wa kashaulili mjini Mpanda wamesema kiongozi ajaye lazima awe na ujasiri wa kupambana na vitendo vya rushwa hususani katika ofisi zilizopo chini ya serikali za mitaa pia mafisadi papa kwani wamechangia kwa kiasi kikubwa watanzania wengi kuishi katika umasikini uliotokea huku wao wakiishi maisha ya peponi.BOFYA HAPA KUTAZAMA ZAIDI
PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp  +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad